Friday, June 20, 2014

Timu ya Biashara United ya Mjini Musoma kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge mjini Dodoma


FULL KUKIMBIZA
Sudi  Hamza akijiandaa kufanya mazoezi
Mshambuliaji wa Biashara United Augustine Mgendi akifanya Mazoezi
Mwenyekiti wa Biashara United Issa Salota naye akijumuika katika mazoezi
    Hapa si dombolo ya solo ni mazoezi ya viungo hayo
Shaban Mganda na Luzinda wakionyoosha viungo
  Kocha wa Timu ya Biashara United Amani Richard Akiongoza Mazoezi
Mgongo ni muhimu kuuonyoosha

Mazoezi ya shingo muhimu
Baada ya Mazoezi ya viungo,Mshambuliaji wa Biashara United Augustine Mgendi akitafakari jinsi ya kuonyesha kiwango zaidi ya wale wa WC kule Brazili,katikati Luzinda akionyesha kiwango huku Mgendi Jr akifurahia mavitu ya Luzinda
                             Sud Hamza (Jamaa anapenda kuuza huyu) akiwa na Jackson


Na Mwandishi Maalum


Timu ya soka ya Biashara United inayoundwa na watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara ipo kwenye mazoezi makali kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini dodoma.


Akiongea baada ya Mazoezi hayo,kocha wa timu hiyo Aman Richard aliesema kwasasa timu yake ipokwenye maandalizi makali kuhakikisha timu yake haiendi kutalii Dodoma huku akiwahakikishia mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kufanya vizuri katika mchezo huo

" Kwasasa tunafanya mazoezi makali sana na lengo ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo,nina imani na kikosi changu na hasa baada ya kumuongeza washambuliai Augustine Mgendi na Stephen Mgendi ambao nina imani wataisaidia timu yangu" alisema Amani

Aliesema mpaka sasa tayari maandalizi ya kuelekea Dodoma yanafanywa kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Musoma Mjini  Mh Vincent Nyerere ambaye ndiyo mwenyeji wa timu hiyo huko mjini Dodoma.

Mbali na mchezo huo dhidi ya timu ya Bunge lakini pia kocha huyo alisema kuwa wanaweza wakacheza mchezo mmoja wa kirafiki katika mkoa wa Singida kama ratiba itaruhusu.,

"Tunategemea pia kucheza mchezo mmoja Singida  kama itawezekana wakati tukiwa njiani kuelekea Dodoma au wakati tunarudi kutoka Dodoma" alisema kocha huyo

No comments:

Post a Comment