Thursday, June 26, 2014

Mtuhumiwa Tarime afariki mikononi mwa PolisiMaandamano ya wananchi wa mji mdogo wa sirari wilaya ya Tarime mkoani Mara  waliotaka kujua chanzo cha mauaji ya kijana mmoja mkazi wa eneo hilo ambaye anadaiwa kukamatwa na Jeshi la polisi na kisha mwili wake kukutwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti katika hospital ya wilaya ya Tarime yamesababisha vurugu kubwa na kusimama kwa shughuli mbalimbali za kijamii kwa saa kadhaa
 
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la kitandika Ryoba anadaiwa kukamatwa siku nne zilizopita na askari wa jeshi la Polisi katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya kwa tuhuma za kukutwa akicheza kamali  lakini tangu siku ya tukio hilo kijana huyo hakupatikana hadi taarifa za kifo zilipowafikia ndugu zake  na mwili wake kuhifadhiwa katika chumba cha Maiti katika hospital ya wilaya ya Tarime
 
Taarifa hizo zilisababisha  wananchi  wa eneo hilo kufanya Maandamano  ikiwa ni njia ya kushinikiza  jeshi la Polisi kueleza chanzo cha kifo  cha kijana huyo ambapo jeshi la polisi liliingia kati kuzima maandamnao hayo hali ambayo  ilisababisha wananchi hao kuifunga barabara kuu ya inayotumika kwa safari za Mwanza,Tarime na nchi jirani ya Kenya  kwa kutumia Mawe lakini pia wakichoma matairi ya Magari.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Tarime Rorya Kamishana msaidizi Mwandamizi Justus Kamgisha amesema Mtuhumiwa huyo kitandika Ryoba baada ya kukamatwa alifikisha kituo cha Polisi kuhojiwa na wakati Mahojiano yakiendelea alidai kujisikia vibaya ambapo nalikimbizwa hospital na wakati anapatiwa matibau akafariki dunia.

No comments:

Post a Comment