Tuesday, February 11, 2014

Mbunge wa Rorya ashinikizwa kugombea tena 2015


Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo majuzi alipata wakati mgumu wa kuendelea na msimamo wake wa kutogombea Ubunge kwa mara nyingine mara baada ya kupewa maneno yenye hisia toka kwa mwenyekiti wa Mkoa mpya wa Geita Joseph Msukuma, aliyeungana na mwenyekiti mwenzake wa CCM Wilaya ya Rorya Samwel Kiboye almaarufu kama 'NAMBA TATU' wakimsii mbunge huyo kutengua ahadi aliyoiweka ya kutogombe tena nafasi ya Ubunge kwa sababu bado wananchi wa jimbo lake wanamkubali kutokana na hatua kubwa za kimaendeleo zilizoonekana kupitia uongozi wake. 
NAMBA TATU ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Rorya aliema kuwa katika uongozi wa Lameck Airo makubwa mengi yameonekana wilayani humo ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara kwa kutumia zana za mbunge na makampuni yake bila kusubiri fedha toka serikalini hali ambayo imesababisha hata barabara ambazo zilikuwa hazipitiki tangu uhuru miaka ya 60 hii leo zimekuwa muhimu na tegemeo kwa masuala mbalimbali ya usafiiri na usafirishaji.
Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma alisema kuwa kwa wale wazawa nawananchi wapiga kura wanatakao kubali uamuzi wa Lameck wa kutogombea tena jimboni humo basi hawayataki maendeleo na ni wale ambao wenye chuki binafsi wasiopenda maendeleo ya Rorya. " Siku zote Lameck amekuwa si msemaji zaidi yeye huzungumza kwa vitendo, hana blaa... blaaa! Hawa ndiyo watu tunao wataka" alisema Msukuma na kuongeza kuwa "Tumekuwa na maprofesa hapa wasemaji wazuuuuuri wakisifika kwa hotuba zao bungeni  jeh wametusaidia nini?" 
"Mimi licha ya kusikia sifa na uchapakazi wa Lameck ni shuhuda tosha wa jimbo hili nilipata nafasi ya kuja hapa Rorya miaka ya 1999 na ya 2000 hapa palikuwa si pa kutamani kulala, ukilala unawaza kesho utaondokaje, na jinsi ya kuondoka ni lazima udamke kuwahi basi la asubuhi ambapo kwa siku kuna mabasi mawili au moja kutokana na kuwa na miundo mbinu mibovu miaka hiyo lakini leo barabara ikiharibuka kidogo matrekta yya mbunge yasiyo subiri bajeti yana sawazisha...Rorya mnataka nini?" Alihoji msukuma.
Makada mbalimbali wa CCM kutoka kata mbalimbali wilayani na vijiji vya Rorya wamehudhuria mkutano huu.
Eneo jingine la wadau katika ukumbi huu wa shule ya Kogalo ulioko katika kata ya Utegi wilayani Rorya, ukumbi ambao umejengwa kwa nguvu ya wananchi wakihamasishwa na mbunge wao Lameck Airo.
Makada wote hawakuafiki suala la Mhe. Lameck kuliachia jimbo wakisema kuwa wataandamana kumtoa kwake akachukuwe fomu muda utakapo wadia.
Sambamba na mada hiyo pia kulikuwa na suala mengine yaliyo jadiliwa ikiwa ni pamoj na suala la kuwajengea uwezo wanachama kuainisha kwa wananchi hatua mbalimbali za kimaendeleo zinazofanyika kupitia serikali ya Chama cha Mapinduzi. 
Maadhimio yalifanywa.
Kisha kusanyiko likaahirishwa.  source Gsengo                                              

No comments:

Post a Comment