Saturday, February 15, 2014

Makamu wa Rais wa Tanzania atembelea Maonyesho ya uwekezaji Mwanza leo

Na G.Sengo-Mwanza
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na wadau wa banda la  Halmashauri ya Jiji la Mwanza kulia akionekana Mmoja kati ya Maafisa wa ofisi za jiji Dr. Kaaya ambaye ndiye msemaji wa banda hilo la maonyesho wakati wa Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa unaomalizika leo jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akimpa mkono wa pongezi Afisa Habari wa Jiji la Mwanza Joseph Mlinzi mara baada ya kupata ufafanuzi wa kina na juhudi za halmashauri kuendelea na mikakati ya kulinda mazingira na kuboresha usafi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal ndani ya banda la TANAPA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akipata maelezo ndani ya banda la Benki ya Standard Charterd .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akipata habari za wawekezaji wa zao la Samaki kiwanda cha VIC FISH Mwanza.
Nyuso za furaha na bashasha za wadau wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Wadau wa NMB.
Ni kama anasema "Aaaah hiyo ni saizi yako mwanangu" Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal sambamba na meza kuu akifurahia hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo wakati akijipima moja kati ya mashati ya vitambaa asili yanayopatikana katika banda hili la Mama Donata Swai.
Mama Donata Swai akionesha moja kati ya pochi zilizo tengenezwa kiufundi kwa kutumia bidhaa za vitambaa na ngozi asili.
Dr. Hozee Hebarist akitoa ufafanuzi wa dawa zake asilia kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal, pindi alipo tembelea banda lake katika maonyesho ya wawekezaji jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment