MUSOMA
Serikali
mkoani Mara imesema itaendelea kusimamia sera na utaratibu uliowekwa katika kupambana
na Changamoto zinazowakabili Wajasiriamali mkoani humo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa
Mkoa wa Mara Bw John Gabriel Tuppa katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa
wilaya ya Musoma Bw Jackson Msome katika Kongamano la wajasiriamali
lililoandaliwa na taasisi isiyo ya Kiseriakli ya Nyangoto Development Group
lililofanyika katika ukumbi wa Magereza manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Bw Jackson Msome kushoto na Bi Ghati Wassira kulia
Katika hotuba hiyo Mkuu wa
Mkoa wa Mara alisema kuwa kumekuwepo na Changamoto mbalimbali ambazo
zinawakabili wajasiriamali mkoani hapa ambapo serikali ya mkoa itaendelea
kusimamia sera na utaratibu ulioweka katika kupambana na changamoto hizo.
"Kama Serikali tunafahamu kuna changamoto nyingi sana ambazo zinawakabili wajasiriamali na kupitia nafasi hii tunasema kuwa tutasimamia Sera na utaratibu uliowekwa ili kusaidia kutatua changamoto hizo" alisema Mkuu huyo wa wilaya
Katika hatua nyingine Mkuu
wa mkoa wa Mara amewataka wajasiriamali hao kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii
CHF kama
njia ya kuimarisha afya zao na familia zao.
Kwa upande wake Katibu wa
taasisi ya Nyangoto Development Group ambaye pia ni Mjumbe wa baraza la UWT
Taifa kutoka mkoani Mara Bi Agness Methew amesema lengo la kuwakutanisha
wajasiriamali hao ni kutaka kutambua changamoto zinazowakabili na kutazama
jinsi ya kuzitatua kwa kushirikiana na Serikali mkoani hapa.
Bi Agnes Methew
"Kukutana hapa sisi wajasiriamali ni katika kukumbushana na kuangalia Changamoto mbalimbali ambazo zimetukabili kwa Mwaka mzima lengo likiwa ni kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo" alisema Bi Agness Methew
Katika hatua nyingne Diwani wa Viti Maalum kutoka wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Bi Ghati Wassira aliwataka Wajasiriamali hao kushirikiana na Serikali kutatua Changamoto zilizopo ili kuhakikisha wanapiga hatua huku akiiomba serikali kuwasaidia Wajasiriamali hao.
Baadhi ya umati wa Wajasiriamali waliojitokeza
Katika Kongamano hilo zaidi ya Wajasiriamali 1000 wanaojihusisha na
biashara tofauti walijitokeza ambapo kiasi cha Shilingi milioni kumi na sita
zilipatikana katika harambee iliyofanyika katika Kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment