Thursday, December 5, 2013

Miaka mitatu jela kwa kujifanya usalama wa Taifa

MUSOMA
Mahakama ya wilaya ya Musoma mkoani Mara imemuhukumu Bw Liso Chacha kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kujitambulisha katika idara mbalimbali zikiwemo za Serikali kama Afisa Mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa.

Licha ya Kujitambulisha katika idara hizo kama Afisa Mwandamizi idara ya Usalama wa Taifa Makao Makuu,Mtu huyo alidanganya Viongozi Wakuu wa Mkoa wa Mara na kujipatia huduma mbalimbali huku akisema ameagizwa na Makao Makuu kufanya kazi Maalum mkoani  hapa.
Katika hukumu hiyo Mwendesha Mashitaka wa Polisi Sajent Stephano Mgaya alisema kuwa June 14 Mwaka huu,Mtuhumiwa huyo alimpigia Simu Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John Gabriel Tuppa na kujitambulisha Kama Afisa usalama kutoka Makao Makuu na hivyo ameagizwa Mkoani Mara kufuatilia Mtandao wa kuuza Risasi kutoka katika kikosi cha Jeshi 27 KJ Makoko na hivyo kuhitaji msaada kutoka mkoani.

Baada ya Kauli ya mtu huyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara aliwasiliana na Mkuu wa Kikosi cha Jeshi Makoko  kwa lengo la kufanikisha Kazi hiyo na kutoa huduma mbalimbali kwa mtu huyo zikiwemo Malazi katika Nyumba ya Maafisa wa Jeshi katika eneo la Tembo Beach  ambapo pia Maafisa wa Jeshi la Wananchi ambapo pia waliwasiliana na Mkuu wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai RCO kwaajili ya kutekeleza agizo hilo.
                                           Bw Liso Chacha (AFISA USALAMA  FEKI)

Katika kutekeleza Agizo hilo vyombo hivyo vya usalama viliteua baadhi ya Maafisa na kuambatana na mtu huyo hadi katika Kizuizi cha Polisi kilichopo Kirumi ili kuweka Mtego na kukamata Magari aliyodai kuwa na risasi kazi ilifanyika kwa Siku mbili bila Mafanikio. 

June 17 Mwaka huu Mtu huyo alifika kwa  Waandishi wa habari Mkoani hapa akijitambulisha kama Afisa Usalama na kutaka  msaada wa wanahabari hao kushirikiana nae katika kufanikisha Kukamata Magari hayo  ambapo walimtilia shaka na kutoa taarifa Polisi.

Akitoa hukumu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Musoma Bw Richard Maganga,amesema Mahakama imeridhishwa na Maelezo ya Mashitaka wakiwemo mashahidi saba kutoka idara mbalimbali ambazo ni  Jeshi la Polisi,Mkuu wa utumishi idara ya usalama wa Taifa ,Waandishi wa habari na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na hivyo kumtia hatiani mtuhumiwa huyo kwa kujifanya Mtumishi wa idara ya Usalama wa Taifa na hivyo kwenda jela Miaka mitatu

No comments:

Post a Comment