Sunday, December 8, 2013

Atakaeleta malumbano na Mgawanyiko ndani ya CCM kukiona

RORYA 
 
Chama cha Mapinduzi CCM wilaya  ya Rorya Mkoani Mara kimesema hakitamvumilia mtu yeyote atakaeonyesha dalili ya kuleta Malumbano na mgawanyiko ndani ya Chama hicho.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Rorya Bw Samweli Kiboye ametoa kauli hiyo katika baraza la vijana wa Chama hicho lililofanyika katika wilaya ya Rorya mkoani Mara.
 
Amesema kumekuwepo na baadhi ya watu ambao wanaleta Malumbano na mgawanyiko ndani ya Chama na hivyo kusababisha Chama kutofanya shughuli zake kama kawaida na hivyo akiwakumbusha kama mambo yataachwa Chama cha Mapinduzi kitafanya vizuri katika Chaguzi zinazokuja
 
"Hatutamvumilia mtu yoyote ndani ya Chama kuendelea kuleta Malumbano na mgawanyiko ndani ya Chama kuruhusu mambo hayo ni kukiua Chama nitapambana nao sasa"alisema Mwenyekiti huyo
 
Bw Bw Samweli Kiboye - Mwenyekiti wa CCM Rorya
 
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amewata vijana hao ambao ni viongozi wa mabaraza ya Vijana katika Kata wilayani humo, kufanya ziara katika kata zao huku akiwapongeza Viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi na kusema kuwa Chama hicho hakitakubali kuona baadhi ya viongozi wa Chama hicho  wanaounga kutukana viongozi wao.
 
"Tunawapongeza sana Viongozi wetu wa juu ndani ya Chama kwasasa wamerudisha uhai wa Chama,tunampongezasana Rais wetu anafanya kazi nzuri na kama tutaacha Malumbano uchaguzi unaokuja kwetu hakuna shida" aliongeza Mwenyekiti huyo
 
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la Vijana UVCCM Rorya
  Baadhi ya wajumbe wa baraza la Vijana UVCCM Rorya
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la Vijana UVCCM Rorya

No comments:

Post a Comment