Friday, November 15, 2013

WANANCHI RORYA WADAI KUVAMIWA NA WANAJESHI WA JESHI LA UGANDA ZIWA VICTORIA

Rorya,MARA

Baadhi ya Wavuvi katika Mwalo wa Uvuvi wa Sota wilaya ya Rorya Mkoani Mara,wanadai kufanyiwa vitendo vya Uharamia na Askari wa Jeshi la Wananchi la Uganda wanaotumia silaha kuwatisha na Kuwanyang'anya Samaki pamoja na Zana zao za uvuvi.


Wavuvi hao walisema kuwa mpaka sasa kuna baadhi ya watu wameuawa na askari hao kwa kuzamishwa Majini,kunyang'anywa Samaki na zana zao za Uvuvi.


'Kiukweli tumechoka na hali hii maana huku ndipo tunapata riziki yetu lakini hawa Wanajeshi wa Uganda wanasababisha Maisha yetu kuyumba maana tunaogopa kwenda ziwani  tunaomba Serikali itusaidie" alisema David Samweli Mvuvi katika Mwalo huo.Naye Bi Mary Otieno alisema kuwa Vijana katika Mwalo huo wanapata tabu kutoka kwa Wanajeshi wa Jeshi la Unganda kuwavamia hivyo wanaiomba Serikali kupitia Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo kuingilia kati tatizo hilo.


Katika hatua nyingine mjumbe wa kamati tendaji wa BMU David toto alisema kuwa kero za Wananchi katika eneo hilo zimekuwa nyingi huku akisema toka mwezi April hadi leo kuwa zaidi ya mitumbwi zaidi ya 30 imevamiwa katika ziwa Victoria.Kwa upande wa Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya kupitia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo  Kamishina Msaidizi wa Polisi Justus Kamgisha,amekiri kuwepo kwa taarifa hizo ambapo jeshi hilo linaendelea kuzifanyia uchunguzi ingawa ameseme taarifa hizo hazielezi  Jeshi la Uganda kushiriki lakini pia akisema  kuwa kuna mawasiliano Mazuri katika idara za Polisi za nchi za Kenya na Uganda.


 " Ni kweli tuliishasikia hayo malalamiko lakini kutoka kwa Wavuvi hao lakini hazipo kimaandishi hapa kwetu,lakini taarifa tulizonazo hazielezi kuwa Jeshi la Uganda linahusika ila matukio ya uvamizi yao"alisema Kamanda Kamgisha

No comments:

Post a Comment