Monday, November 18, 2013

SERIKALI YATAKIWA KUKABILIANA NA TATIZO LA NJAA SERENGETI

SERENGETI -MARA

Serikali imetakiwa kuchukua hatua za haraka ambazo zitasaidia kukabiliana na tatizo la njaa katika wilaya ya Serengeti Mkoani Mara lililosababishwa na ukame pamoja na uvamizi wa tembo katika baadhi ya maeneo ya Makazi ya watu  na Mashamba.

Baadhi ya Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoani Mara walitoa kauli hiyo katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ambapo suala hilo lilionekana kutumia muda mrefu katika kulijadili.

    Mkurugenzi halmshauri ya Musoma kushoto na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Ng'oina.
Walisema  kumekuwepo na tatizo la njaa katika wilaya hiyo ambalo limesababishwa na Ukame lakini pia  kuwepo kwa tembo wanaoingia katika Makazi ya watu na Mashamba na kufanya uharibifu wa Mazao katika Mashamba jambo ambalo limesababisha tatizo kubwa la njaa.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Bw John Ng'oina alishauri kuwepo kwa uzio katika maeneo ya hifadhi huku Mkurugenz wa Halmashauri hiyo Bi Goody Pamba alihimiza kulima mazao yanayokomaa haraka na Wafugaji kuuza baadhi ya Mifugo na kununua Chakula.
Katika kikao hicho cha Madiwani kilieleza kuwa kutakuwepo na Mkakati wa kuwepo kwa kikao  cha wadau wa Maliasili katika kujadili Masuala mbalimbali likiwemo la tembo kuingia katika Makazi ya watu.

No comments:

Post a Comment