Wednesday, October 16, 2013

HIVI NDIVYO KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA TIGO ILIVYOAZIMISHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MJINI MUSOMA KWA KUWA KARIBU NA WATEJA WAKE

 BIDHAA MPYA GHARAMA NAFUU FIKA DUKA LA TIGO MUSOMA


 Bi Pilila Kavishe

 HAPA KAZI TU




 ZAWADI KW WATEJA KAMA KAWAIDA
 MFANYAKAZI WA TIGO MUSOMA AKIENDELEA NA MAJUKUMU



 AFISA HUDUMA KWA WATEJA WA TIGO Bi Pilila Kavishe  AKITOA ZAWADI KWA WATEJA WA TIGO KATIKA MAAZIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 14 BAADA YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE


Kampuni ya Tigo Mkoani Mara imesema itaendelea kuwaunganisha Watanzania wote  kupitia Mawasiliano yaliyo bora ikiwa ni kuenzi misingi ya umoja na Mshikamano iliyoasisiwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .
Hayo yalielezwa na Afisa huduma kwa Wateja wa Tigo Bi Pilila Kavishe katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 14 ya kifo cha Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alisema kuwa kampuni ya Tigo itaendelea kushirikiana na wateja wake katika shughuli mbalimbali za  Kijamii ikiwa ni njia ya kutambua na kuthamini Mchango wa wateja wake kwa Kampuni hiyo.
Meneja huyo alidai hakuna kitu ambacho kinaweza kuwaunganisha watu kwa haraka kama mawasiliano hivyo kampuni hiyo itaendelea kumuenzi mwalimu Nyrere kwa kufanikisha mawasiliano ya uhakika.
Alisema kampuni ya tigo inaheshimu misingi ya Mwalimu Nyerere na katika kuienzi ni kuhakikisha Wananchi walio wengi wanafikiwa kwa mawasiliano na kuwaweka pamoja.
Kwa upande wao wateja wa tigo walioshirikiana na kampuni hiyo na kupokea zawadi mbalimbali kutoka tigo walisema kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhaakikisha huduma bora inapatikana kwa wateja ikiwemo mawasiliano ya uhakika na kuwataka kuto kurudi nyuma.
Mmoja wa wateja wa tigo alijitambulisha kwa jina la ingali Daudi alisema wameishukuru kampuni ya tigo kwa kufanya kumbukumbu ya muasisi wa Taifa kwa kuboresha mawasiliano mkoani mara na nchini kote kwa kuwa ndio uzalendo halisi.  

No comments:

Post a Comment