Monday, September 2, 2013

RAIS KENYATTA AZIDI KUWAPA UTAJIRISHO WANANCHI WA KENYA

RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema licha ya wakazi wa Taita Taveta kutompigia kura lakini kwa kuwa aliahidi Wakenya kuwa akishinda atashughulikia tatizo la ardhi,ameanza na mkoa huo wa Pwani kwa kutoa hati za kumiliki ardhi ili kuhakikisha wananchi wanapambana na umaskini.

"Najua hamkunipigia kura ...wala hiyo si uongo...mlichagua watu tofauti na chama ya Jubillee ...hiyo ni haki yenu...sisi tuliahidi wakenya ..hivyo nimeanza na mkoa huu kugawa hati ...maana ardhi ni maisha ...ili tuondokane na umaskini lazima tutekeleze ahadi zetu.....nataka baada ya miaka mitano watu mil.3 wamepata hati kwa gharama za serikali....hii nafunga mjadala wa watu kuja kuomba kura kwa matatizo ya ardhi waje na mambo mengine"amesema.

Amesema wanataka kubadilisha maisha ya Wakenya kwa kutimiza ahadi walizoahidi,"ni miezi mitatu toka tumeanza kazi...na tumeanzia mkoa wa Pwani maana matatizo yake yanajulikana,nimemwambia Waziri wa ardhi kuhakikisha anaandaa hati zaidi ...leo nakabidhi 19,103 ...lazima tuwatumikie watu wetu bila kuangalia yeye ni chama gani maana wote tumechaguliwa na Wakenya na tujenge Kenya yetu"anasema Rais.

Makamu wa Rais William Ruto amesema mkoa huo una neema ya Madini,na maliasili hivyo wamepeleka sheria bungeni ambayo itasaidia wananchi kunufaika na madini ,na kuwa wananchi watakuwa wanufaika wa kwanza,jimbo na serikali kuu.

"Suala la Ujangili tutahakikisha tunaumaliza kabisa ..kwenye bajeti tumetenga ksh,mil.770 kwa ajili ya utalii...tutafanya operesheni kali kuhakikisha tunaondoa ujangili....na lengo letu ni kuelekeza nguvu kujenga uchumi wa watu wetu...tutatumia kilimo cha umwagiliaji pia ili kuondokana na aibu ya njaa na kuomba chakula"amebainisha.

Ili kuhakikisha wananchi wananufaika mapato yote yanayotoka eneo hilo asilimia 32 inabaki kwenye jimbo badala ya asilimia 15 iliyoandikwa kwenye katiba,fedha hizo zitasaidia kujenga uchumi wa jamii kwenye jimbo.

Waziri wa ardhi Charty Ngilu amewaambia wananchi kuwa mpango uliopo sasa ni kuwaweka wananchi wote kwenye senta moja watakapojengewa makazi na kupewa huduma zote ,kila mmoja atapewa hati ya kumiliki eneo lake,na mashamba yao yatabaki kwa kilimo badala ya kuishi mashambani.

Baadhi ya viongozi wa jimbo hilo akiwemo gavana alisema kwa miaka 52 hayo hayakuwahi kutokea lakini kwa miezi mitatu Kenya inabadilika kwa kuwajengea  uwezo wa kiuchumi wananchi wa taifa hilo.

Wamesema siasa zimekwisha sasa ni kufanya kazi kujennga Kenya,na wanaopiga siasa kuwa kazi anazofanya Rais za kugawa hati zilitakiwa kufanywa na karani wananchi wawapuuze.

No comments:

Post a Comment