IKIWA Tanzania leo inaungana na ulimwengu mzima kuazimisha siku ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya,jamii hususani vijana wametakiwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya mbayo yamekuwa yakiathiri nguvu kazi ya Taifa na kuwafanya vijana wengi kuishi katika hali hatalishi.
Rai
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Jamii Information Network
linaloshughulika na utoaji elimu katika utambuzi wa mambo mbalimbali
yenye kujenga jamii Augustine Mgendi alipokuwa akizungumza na Blog hii
namna vijana wengi walivyoathirika kutokana na matumizi ya
madawa ya kulevya.
Amesema
vijana wengi ambao ndio tegemeo katika ujenzi wa Taifa wamejitumbukiza
katika matumizi ya dawa za kulevya na hivyo kushindwa kushiriki ipasavyo
katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo huku wengi wao
dawa hizo zikiwatuma kushiriki katika vitendo vya uhalifu.
Mgendi
amedai ikiwa Tanzania inaungana na mataifa mengine Duniani katika
kupinga matumizi ya dawa za kulevya pia inawajibu ya kupanga mikakati
kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutoa elimu
katika sehemu mbalimbali juu ya athari kubwa zinazotokana na dawa za
kulevya ili kila jamii hasa vijana waweze kuepukana na matumizi yake.
Amesema
wapo vijana ambao wanajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya bila
kufahamu athari zake na wengine kwa kuiga wale wanaotumia hali ambayo
inafanya kuongezeka kwa idadi kubwa ya vijana wanaojiingiza katika
matumizi ya dawa hizo.
Akitolea
mfano wa dawa za kulevya aina ya bangi (Cannabis) kitaalam inamfanya
mtumiaji kukosa umakini na kushindwa kufanya vitu vinavyohitajika na
uwezekano mkubwa kupata kansa na kuharibu mapafu kutokana na matumizi ya
muda mrefu na hata kupelekea kuzaa vilema.
"Zipo
athari nyingi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi
ambayo vijana wengine wamejitumbikiza huko,lakini wapo wengine kutokana
matumizi ya bangi kunawapelekea kuchanganyikiwa na kupumbaa kwa ufahamu
hivyo kunahitajika elimu.
"Licha ya bangi,dawa za kulevya aina ya (Narcoticks) ambapo ndani yake
kuna dawa kama Heroine,darvon,hydrocodone,codeine vijana ujiingiza
kuzitumia bila kujua athari zake na pengine bila kupata elimu hivyo
kuendelea kuangamiza Taifa.
"Moja
ya athari ya dawa hizi ni kupoteza fahamu,kuugua ugonjwa wa kifafa na
hata kifo pale utakaozidisha kipimo,sasa kama elimu haitatolewa kwa
vijana kwa kuzitambua athari zake tutapoteza vizazi vingi,"alisema
Mgendi.
Amesema
kutokana na gharama kubwa ambazo hutumika kurudisha hali ya kawaida ya
mtumiaji wa dawa za kulevya,Shirika la Jamii Information Network kwa
kushirikiana na wadau wa Mashirika mengine ya kijamii wamekusudia kutoa
elimu ili kuweza kuwaepusha vijana na kujiingiza katika matumizi ya dawa
za kulevya ambapo wameanda Kongamano kwa vijana mwezi August mwaka huu katika kutoa elimu kwa zaidi ya Vijana 200 wa Manispaa ya Musoma
No comments:
Post a Comment