Friday, May 10, 2013

WAFANYABIASHARA MKOANI MARA WALALAMIKIA SUMATRA MARA


UMOJA wa wafanyabiashara wa Usafirishaji mkoani Mara,wamelalamikia kitendo cha Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini SUMATRA mkoa wa Mara kwa ukiukwaji wa sheria namba 8 ya mwaka 2007 ya Mamlaka hiyo kwa kuruhusu na kupangia safari magari ambayo hayana leseni ya kusafirisha abiria.

Katika barua yao iliyoandikwa kwenda kwa Meneja wa SUMATRA mkoa wa Mara ambayo imedai inashangazwa na Mamlaka hiyo kukiuka sheria ambazo inazisimamia kwa kuruhusu mambo ambayo yanakwenda kinyume cha utaratibu kwa kuruhusu magari hayo na hivyo kuwanyonya wenye leseni halali.

Barua hiyo imesema  kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilalamikia suala hilo kwa kufikisha taarifa maeneo husika lakini hakuna hatua zozote ambazo zimekwisha kuchukuliwa na Mamlaka yoyote kutokana na ukiukwaji wa sheria.

Sehemu ya barua hiyo imesema hata walipoona Sumatra inashindwa kulichukulia hatua suala hilo wamekwenda katika vyombo vingine ikiwemo kikosi cha usalama barabarani lakini hadi leo hakuna hatua iliyochukuliwa.

Katika barua hiyo ambayo nakala yake ilipelekwa kwa kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mara pamoja na ofisi ya Mamlaka ya Mapato TRA ililikalili gari namba T 930 BVW aina ya Toyota Costa linalofanya safari kati ya Majita na Musoma linalodaiwa kuwa la mfanyabiashara maarufu mkoani Mara limekuwa likifanya biashara ya usafirishaji wa abiria kwa muda mrefu bila kufuata taratibu za kisheria.

Dereva hao walidai huenda kuna kitu cha chini ambacho kinafanyika baina ya wamiliki wa magari hayo pamoja na maofisa wa Sumatra na mamlaka nyingine kwa kuwa suala hilo licha ya kulilalamikia lakini bado wamelikalia kimya na kushindwa kuchukua hatua zozote.

 Akizungumza na kuhusiana na malalamiko hayo,Meneja wa Sumatra mkoa wa Mara Bw Michael Rogers,amekili kuwepo kwa gari lililotajwa namba zake likifanya kazi bila kufuata utaratibu na tayari ameshawasiliana na vyombo vingine vya usalama kufatilia malalamiko hayo.

Hata hivyo amekiri kuwa gari namba T 930 BVW Toyota Costa imelikuta likiwa limebeba abiria maeneo ya Musoma Mjini tayari kuelekea Majita Busekera Wilaya ya Musoma Vijijini huku likiwa halina stika za Sumatra wala bima na nikaliamulu kushusha abiria mbele ya polisi na kupelekwa kituoni kwa hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment