Thursday, May 23, 2013

NBC YADHAMINI YATOA SOMO LA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA TANGA


Na Mwandishi Wetu
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia kitengo chake cha Huduma za Kibenki zinazofuata kanuni za kifedha za Kiislamu inatarajia kuanzisha huduma ya mikopo kwa wafanyakazi ‘Islamic Group Finance’  kabla ya Septemba mwaka huu.

 Akizungumza wakati wa semina ya siku moja ya wanawake wajasiriamali wa Kiislamu jijini Tanga jana, Mkuu wa Islamic Banking wa NBC, Yassir Masoud alisema lengo la kuanzishwa kwa huduma hiyo ni kutoa fursa za mikopo kwa wateja wao wanaohudumiwa kwa kufuata kanuni za dini hiyo.

 Masoud aliwaambia wanawake waliohudhuria semina hiyo kwamba ili waweze kujikwamua kiuchumi, wanahitaji kujifunza mbinu za biashara, akisisitiza kwamba hata mafundisho ya Kiisllamu yanatoa maelekezo kuhusu utafutaji wa riziki.

 ”Uislam umehimiza mambo ya uwekezaji, Uislamu unahimiza masuala ya mali maandiko yakisema kwamba kutafuta riziki ni sawa na kutafuta fadhila za Mwenyezi Mungu,” alisema.
 Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga bibi Chiku Galawa aliwahimiza wanawake mkoani humo kujizatiti kwenye ujasiriamali ili kusaidia juhudi za serikali katika kuinua maendeleo yasiyoridhisha ya mkoa huo.

Alisema kuwa kwa kupitia semina hiyo, NBC imefungua njia mpya yenye matumaini kwa wanawake wa Tanga, njia ambayo mashirika mengine yanapaswa kuifuata.

“NBC ni moja kati ya benki kongwe yenye mtanda mpana kuliko zote nchini na imekuwa mstari wa mbele ikishirikiana na watu mbalimbali katika kuboresha maisha ya Watanzania,” alisema.

Katika siku za hivi karibuni, NBC imekuwa ikiwekeza zaidi katika kuelimisha jamii, hususan wajasiriamali kupitia semina na warsha mbalimbali huku ikishirikiana na makampuni mengine.
Mwishoni mwa mwaka jana, benki hiyo iliandaa mkutano wa wajasiriamali wadogo wadogo wa jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano na shirika lisio la kiserikali linalojishughulisha na vijana, YESi.

NBC pia ni wadhamini wa Top 100 Midsize Companies Survey ambayo inaendeshwa kwa ushirikiano na KPMG kuyasaka na kuyazawadia makampuni ya kati yanayokuwa kwa kasi.
“Sekta ya Biashara ndogo ndogo na za kati ni muhimu katika kukuza uchumi nchini, na ni sekta inayoweza kutoa nafasi za ajira kwa wananchi wengi. NBC wametambua hilo,” alisema.

Aliishukuru benki hiyo na kuishauri iendelee kutoa mafunzo kwa wahusika wa sekta hiyo na kuwawezesha wajasiriamali kukuza biashara zao na hatimaye kuinua uchumi wa nchi.

Rais Kikwete amwapisha Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria na Mabalozi Wapya wanne

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal  na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wapya waliopaishwa leo ikulu jijini Dar es Salaam.aliyesimama mbele kushoto no Balozi Liberata Mulamula anayekuwa Balozi Mpya wa Tanzania nchini Marekani.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi mpya wa Tanzania Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga,Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva Balozi Modest jonathan Mero na Balozi mpya wa Tanzania katika falme za Kiarabu(UAE)Mbarouk Nassor Mbarouk.Kabla ya uteuzi Balozi Liberata Mulamula alikuwa msaidi wa Rais Masuala ya kidiplomasia na aliwahi kuwa katibu mkuu wa nchi za  Maziwa Makuu.(picha na Freddy Maro) Balozi Kilumanga-Commoro Akiapa Balozi Masilingi-Uholanzi akiapaBalozi Masilingi-Uholanzi akiapa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (UAE) akiapaBalozi Mbarouk Nassor Mbarouk (UAE) akiapa Balozi Mero-Geneva akiapaBalozi Mero-Geneva akiapaJaji Aloycius Mujuluzi akiapaJaji Aloycius Mujuluzi akiapa

No comments:

Post a Comment