Tuesday, May 21, 2013

J Martins asema AY ni kama kaka


Staa wa muziki kutoka Nigeria J Martins kwenye exclusive interview na Millard Ayo, amesema msanii Mtanzania AY ni kama kaka yake ndio maana hatojihusisha kumdai pesa yoyote kwenye ishu kama za kufanya kolabo pamoja.

J Martins ambae tayari amerekodi kolabo na wasanii Watanzania, Ommy Dimpoz na Mwana FA, amesema alifanya hivyo bure kwa heshima ya AY ambae ndio msimamizi wa wasanii hawa.

Namkariri akisema: "Ay ni kama kaka yangu, anaweza kuja Lagos nyumbani kwangu na akafanya chochote kama ndugu, sio mtu ambae nimekutana nae jana usiku... ndio maana siwezi kumtoza pesa ya kufanya kolabo manake ni mwanafamilia."

Baada ya kurekodi kolabo kwenye studio za MJ Records Dar es Salaam, chini ya producer Marco Chali, J amesema huwa hachaji pesa kwa msanii yeyote anaetaka kufanya nae kolabo ila uongozi unaomsimamia yeye na 2Face unaweza kufanya hivyo na ni sahihi manake ni sehemu ya utaratibu na hawezi kupinga maamuzi hayo.

Kingine alichosisitiza ni kwamba pia huwa hafanyi kolabo ovyo ovyo, yani hafanyi hivyo wakati wote.. huwa anachagua sana kwa kila single anayofanya.

J amekiri kwamba pamoja na wasanii wengi wa Nigeria sasa hivi kuwa na ndoto za kufanya kolabo sana na mastaa wa muziki kutoka Marekani, yeye ndio msanii ambae amefanya kolabo zaidi ya kumi na wasanii tofauti wa Afrika akiwemo Fally Ipupa, Cabo Snoop, Ommy Dimpoz, Mwana Fa na wengine.

No comments:

Post a Comment