Sunday, May 26, 2013

IRINGA NI SHWARI MACHINGA WAPINGA KUTUMIKA KISIASABaadhi ya maduka eneo la Mashine tatu mjini Iringa yakiwa yamefungwa kwa hofu ya kutokea vurugu ,ambazo hata hivyo hazijatokea baada ya machinga kugoma kutumiwa kisiasa
Hali ilivyo eneo la Mashine tatu mjini Iringa


Haya ni maadishi yanayosomeka HATARI yaliyochorwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana kama sehemu ya kuwatisha wananchi na kuhamasisha vurugu kabla ya jeshi la polisi kuweka ulinzi mkali eneo hilo

Wafanyabiashara wa maduka ya mchele eneo la mashine tatu wakiendelea na biashara zao kwa utulivu zaidi leo

Hili ndilo eneo la mashine tatu kama linavyoonekana mchana huu baada ya machinga kukubali kuheshimu sheria ya mipango miji na kuachana na mvutano usio na tija kwao

Amani na utulivu warejea eneo la Mashine tatu mjini Iringa ,wananchi waendelea na shughuli zao kama kawaida leo ,machinga wakubali kutii sheria
Askari wa FFU akiwa katika ulinzi eneo la mashine tatu leo ambapo hali imetulia zaidi
Askari wa FFU mjini Iringa akipita eneo la mashine tatu ambako machinga walipanga kufanya biashara na vurugu leo ila hali ya amani imetawala zaidi eneo hilo
Askari wa FFU wakiwa kazini leo eneo la mashine tatu
Ulinzi waimarishwa eneo la mashine tatu ,machinga wakubali kufanya biashara eneo la Mlandege kama awali
Hivi ndivyo hali ilivyo eneo la mashine tatu leo ni amani na utulivu kwenda mbele hakuna mabomu leo
Leo ni amani zaidi Iringa hakuna vurugu zozote
Hali ya amani na utulivu imerejea mjini Iringa baada ya machinga kukubali kuendelea na biashara zao katika eneo la Mlandege ambalo uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa iliwatengea wamachinga hao .

Uchunguzi uliofanywa  katika eneo hilo umeshuhudia kuwepo kwa amani zaidi na wafanyabiashara waliokuwa wamefunga maduka yao kuhofia amani kuvurugika wameonekana wakifungua maduka yao huku machinga ambao walihamasishwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kurejea eneo hilo wakionyesha kupuuza ushauri huo wa mbunge na kuelekea Mlandege kama Manispaa ilivyowataka .

Baadhi ya machinga wamesema kuwa suala hilo la machinga kurudi eneo hilo lipo kisiasa zaidi na kuwa kama si mbunge kuwahamasisha machinga hao kupitia mikutano yake hakuna machinga ambae angerejea eneo hilo kwani wengi wao kuwepo Mlandege walionyesha kukubali .

Hata hivyo machinga hao wamesema kuwa hata waliofanya vurugu wiki iliyopita si machinga ni wahuni kutoka maeneo mbali ambali ambao walifanya fujo hizo na kuwa machinga kama machinga hana nafasi ya kufanya vurugu zaidi ya kutafuta pesa.

Pia uchunguzi unaonyesha jeshi la polisi mkoa wa Iringa kujipanga vema kwa siku ya jana usiku na leo ikiwa ni pamoja na kuwakamata baadhi ya watu ambao walikuwa wakitoa kauli za kichochezi katika vijiwe mbali mbali .

Huku askari wa FFU kwa mara ya kwanza usiku wa kuamkia leo walionekana wakiweka ulinzi mkali katika maeneo mbali mbali ya mji likiwemo eneo la soko la Kihesa ,Mlandege, Mashine tatu na maeneo mengine mengi hali iliyopelekea vikundi vya vurugu kutoweka ghafla mjini Iringa na wale waliokuwa wamepanga kuvuruga amani kuamua kusitisha mpango huo.

Wakati huo huo mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma amewapongeza machinga kwa kukubali kurejea eneo la Mlandege ambalo uongozi wa Manispaa ya Iringa ulikuwa umewapangia na kuwa hekima iliyoonyeshwa na machinga hao inapaswa kuigwa na makundi mengine ambayo yamekuwa yakichochewa kufanya vurugu kutokana na matatizo yao.

"Kweli napenda kuwapongeza sana machinga wametumia busara sana baada ya kikao chao na mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa kuhusu kutafuta suluhu lao .....bila shaka wameonyesha kumsikiliza na kumheshimu vema meya na mimi kama mkuu wa mkoa nawaahidi kuwa suala lao litatafutiwa uvumbuzi wa kudumu nawaomba wawe na subira na kuepuka kutumiwa na wana siasa katika suala lao"
 na mtandao huu wa www.matukiodaima.com

No comments:

Post a Comment