aliyekuwa waziri wa elimu na utamadubi
mwaka 2000 hadi 2001 Joseph Mungi, akizungumza na wanahabari (hawapo
pichani) juu ya mustakabari wa elimu nchini.
HATIMAYE waziri
wa zamani wa elimu na utamaduni Joseph Mungai, ameiponda kamati
ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza matokeo
mabaya ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012 ambayo yaleta historia
mbaya kwa Taifa.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani Iringa, Mungai aliyeiongoza Wizara ya Elimu na
utamaduni wakati wa serikali ya awamu ya tatu mwaka 2000-2005, sambamba na kuwa
Mbunge wa Mufindi Kaskazini, alisema inafaa matokeo ya mitihani yawe
yanatangazwa kwa uwazi hata kama ni mabaya tofauti na ilivyo sasa.
Aidha
katika barua yake ya wazi ya Machi 29 mwaka huu yenye kumbukumbu namba
JJM/2013/ELIMU/19 iliyoandikwa kwenda kwa Mwenyekiti wa Tume ya Elimu
iliyoundwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wa
kidato cha nne mwaka 2012, Mungai ameitaka tume hiyo irejee utafiti
uliofanywa na Wizara ya Elimu na Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mwaka 2010 ambayo ilifanya utafiti kudadidi sababu
za ufaulu mbaya ambayo pia serikali kushindwa kuusoma utafiti huo bungeni
ikihofia madudu yaliyogunduliwa.
Katika
barua hiyo, Mungai amehoji sababu za kutoweka bayana ukweli licha ya taarifa
hiyo ya utafiti kuwapo kwenye maktaba za Wizara na kwamba
anayoyasema hivi sasa ameyapata kutoka taarifa moja isiyo ya siri ndani ya
Wizara ya Elimu.
Ametaka kamati hiyo kutotumia
muda na fedha nyingi katika shughuli hiyo ya utafiti ambao majibu yake yapo
katika utafiti uliofanywa na kugundua mapungufu ambayo yalifichwa.
Mungai
ameitaka tume hiyo ieleze wazi wazi kwamba Taasisi ya Elimu (TIE), iachiwe
masuala ya kutekeleza wajibu wake wa kisheria chini ya sheria ya elimu ya
mwaka 1995 ya kuandaa na kuboresha mitaala.
“Tume
ya Waziri Mkuu (Pinda) ifanye kwanza rejea ya maandiko ya Wizara ya Elimu
ambayo ni Nyaraka za Elimu za mwaka 1999 hadi 2005 na Sheria ndogo za Elimu au
kanuni za elimu zilizotungwa kuyapa maboresho hayo uzito wa kisheria
yamepelekwa nyaraka za kale kabla ya wakati wake…Hii itasaidia badala ya
kutumia muda mwingi na fedha nyingi kugundua upya gurudumu,” inasema sehemu ya
barua hiyo ya wazi kwenda kwa Tume ya Waziri Mkuu.
Hata
hivyo akijibu maswali ya wanahabari juu ya kukinzana kwa mitaala, kama ipo ua
laa, Mungai alisema mitaala ipo ila tatizo ni namna inavyotumika, huku
akimkejeri Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia kuhusu kauli yake
aliyoitoa Bungeni miezi michache iliyopita kwamba nchi inaongozwa bila mitaala
ya elimu.
Amesema kauli ya Mbatia haikuwa
na ukweli kwa vile mitaala hiyo ipo isipokuwa kuna ‘madudu’ katika
taasisi za umma zinazohusina na elimu.
Pia
amesema Mbatia aliitoa kauli yake bungeni pasipo kufanya utafiti wa kina na
kwamba hata wapinzani wa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wanajua kwamba
wanasiasa huamua bila kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri wa kitaaluma
kuhusu elimu ya taifa letu.
“Kwa
hiyo mimi ninaimbia tume ya Waziri Mkuu kwamba utaratibu sahihi wa kupanda
madarasa kwa kufaulu uliowekwa na Waraka wa Elimu namba moja na namba mbili wa
mwaka 2002 urejeshwe na uimarishwebila kuchelewa ambayo mwalimu mkuu siku zote
anayo madaraka ya kukaririsha kama mwanafunzi hajazijua zile ‘K’ 3 yaani
kusoma,kuandika na kuhesabu,”Alisema Mungai.
Hata hivyo amewataka wanasiasa
kuacha tabia ya kuingilia masuala yenye maslahi kwa Umma hasa elimu, pasipo
kufanya utafiti kwa kuwashirikisha wataalamu waliobobea katika masuala y elimu.
Amesema pia michezo mashuleni
inachangia kwa kiwango kikubwa kudumaza kama siyo kudidimiza elimu nchini, na
kuwa ndiyo sababu kubwa ya yeye kuindoa Umishutamta na umiseta katika awamu
yake, kwa madai kuwa wanafunzi na walimu walilazimika kutumia zaidi ya siku 70
katika michezo na hivyoi wanafunzi kupoteza vipindi (Syllabus) .
Ameitaka wizara kuendeleza
michezo pasipo kuathiri vipindi vya wanafunzi darasani, kwa kufanya michezo
wakati na baada ya masomo, ili kutoathiri taaluma ya elimu.
Amesema kuna haja wadau
wanaotoa maoni yao wakasikilizwa pasipo viongozi kuwa na dhana potofu juu ya
ushauri unaotolewa na wadau wa elimu, kwani hatua hiyo ni utekerezaji wa ombi
la waziri mkuu la kuwataka wadau wa elimu kutoa maoni yao ili kuchangia
uboreshaji wa sekta hiyo nyeti.
No comments:
Post a Comment