Serengeti
ASKARI
wawili wa jeshi la polisi katika mkoa wa Kagera,wamekamatwa wakiwa na meno ya
Tembo katika hifadhi ya taifa ya Serengeti mkoani Mara.
Mkurugenzi
mkuu wa Tanapa Allan Kijazi,akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema
askari hao walikamatwa juzu jioni na akari wa hifadhi ya Serengeti kwa
kushirikiana na polisi wa kituo cha Mugumu.
Alisema
askari hao walifanikiwa kuwakamata askari wenzao wakati wakipeleleza kuhusu
matukio ya wizi wa nyara za serikali hivyo kuwakuta na vipande vya meno ya
tembo ambavyo vikiunganishwa yanafikia meno mazima sita.
Alisema
majangiri hayo ambao ni askari polisi walikuwa wakisafirisha meno ya tembo
kutoka kijiji cha Bunchugu wilayani Serengeti kwenda Mugumu mjini kwa kutumia
pikipiki mbili.
Hata hivyo
Kijazi alisema polisi na askari wa wanyamapori wamekamata mmoja ya watu
walikuwa wakiesha pikipiki na mwingine aliyekuwa amebeba mzigo huo huku
mwingine akikimbia.
Alisema
watuhumiwa hao baada ya kukamatwa waliwapeleka askari kwa matajiri walikuwa
wakipelekewa mzigo katika hotel ya Galaxy ambapo pia wamekamatwa pamoja na gari
ndogo.
Alisema
baada ya kuhojiwa watu hao wamegundulika kuwa wao ni askari polisi mwenye cheo
cha Koplo na Konsitebo kutoka Biharamulo mkoani Kagera.
Alisema
baada ya kufanywa kwa mawasiliano na mkuu wa polisi katika eneo walikotoka
wamekili kuwa ni askari wake huku akishangazwa kukatwa katika eneo la Serengeti
mkoani Mara.
Katika simu
zao imeonyesha kuwa walikuwa na mawasiliano na watu walioko kwenye mtandao wa
mkubwa wa ujangiri wa meno ya tembo.
“Huu mtandao
ni mkubwa san asana na wazi sasa imebainika hata Yule faru George aliyepokelewa
na Rais Kikwete ndo walihusiku kumuuawa kwaajili ya kuchungua nyara zake…hii ni
hatari kwa kwenzetu polisi kushiriki katika kufanya hujuma kwa taifa
lao”alisema Kijazi.
Alisema
baada ya mahojiano yanayofanyika kituo kikuu cha Mugumu wilayani Serengeti
taarifa kamili ya majangiri hao itatolewa.
“Tunaomba
ushirikiano na wananchi ili kuhakikisha kuwa tunalinda rasilimali zetu…kwani bila
ushirikiano kamwe hatuwezi kufanikiwa”alisema Kijazi.
Mkuu wa
jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema,amethibitisha kukamatwa kwa askari hao
huku akisema hatua hiyo imetokana na ushirikiano mzuri kati ya askari polisi na
watumishi wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti SENAPA ambao umewezeshwa kukamatwa
kwa askari.
IGP Mwema
akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana kwa njia ya simu alisema kuwa
ingawa kitendo hicho kimelifedheesha jeshi la polisi lakini kamwe jeshi hilo
halitakata tama kwa kuwaondoa kazini askari wake wanakwenda kinyume na maadili.
“Jeshi la
polisi tumekuwa na ushirikiano mzuri na wenzetu wa Tanapa hata kukamatwa kwa
askari hawa wawili kumetokana na ushirikiano uliopo kati ya polisi Mugumu na
watumishi wa hifadhi ya Serengeti”alisema IGP Mwema kwa njia ya simu.
Alisema
jeshi la polisi kwa kushirikiana na Tanapa limekuwa likiendesha mazoezi
mbalimbali ya kupambana na ujangiri katika maeneo mbalimbali nchini hivyo kamwe
haliwezi kurudi nyuma kwa utovu wa nidhamu ambao umeonyeshwa na askari hao.
“Ndani ya
jeshi tuna progarammu ya kutoa zawadi kwa kila askari wanaofanya vizuri katika
kupambana na uharifu pia kwa wale waokwenda kinyume tumekuwa tukiwachukulia
hatua ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi”alisema Mwema.
“Mpango wa
kutii sheria bila shuluti pia unawalenga askari hivyo nakuhakikishia kuwa
lazima tutalisafisha jeshi letu la polisi kama kuna askari anajijua hawezi
kwenda na kasi hii ya sasa ni vema akajiondoa mwenyewe”alisema IGP Mwema.
Hata havyo
ameomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kupambana na vitendi vya
uhalifu katika maeneo yao na ujangiri katika hifadhi za taifa.
Kuhusu maua
ya kikatili yanayoendelea mkoani Mara,IGP amesema tayari jeshi la polisi
limetuma timu maalum ya kuendesha oparesheni maalum ambayo itahakikisha
inakomesha unyama huo.
“Tulituma
timu ya kwanza ya kukusanya taarifa sasa tumetuma timu kubwa ya kufanya
oparesheni kubwa na ya aina yake ili kuhakikishaji kila alihusika anakamatwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria lakini pia ni vyema wananchi wakatoa
ushirikiano wakati wa kazi hiyo kubwa na vikundi vya ulinzi pia vifanye kazi
yake”alisema mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini.
No comments:
Post a Comment