WAUUGUZI WA HOSPITALI |
Na Shomari Binda
Musoma
MKUU wa Mkoa wa Mara John Tuppa aliwataka Wajumbe wateule wa Bodi ya Hospitali ya Mkoa huo kufanya mabadliko katika Hospitali hiyo kwa kuweka
miundombinu ,wataalam,vitendea kazi,uongozi na usimamizi wa kutosha ili
kuiwezesha kutoa huduma za afya zinazokidhi kiwango cha hospitali ya Rufaaa ya Mkoa.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizundua bodi ya hospitali hiyo katika ukumbi wa uwekezaj uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambayo hivi karibuni ilitangazwa na Waziri wa Afya Dk,Hussen Mwinyi.
Alisema endapo bodi hiyo itasimamia kikamilifu shughuli
zake kutakuwepo na mabadiliko ambayo ni ya faraja na
uchangamfu kwa wananchi kutokana na umuhimu wake wa kutoa huduma iliyo
bora na kutibu magonjwa
yaliyoshindikana.
Mkuu huyo aliwahasa wajumbe hao kujiepusha
na migongano isiyo ya lazima na kutoingilia shughuli za madaktari bali
wafanye kazi yao kwa kufuata maadili
mema katika kuboresha huduma ili
hospitali hiyo iweze kufikia kiwango cha rufaa katika kuimarisha utendaji kazi
wa watumishi ili kuleta tija .
“Kuimarisha utendaji kazi wa watumishi ili kuleta tija na kuwepo usimamizi kutoka
uongozi wa juu ,kwa kuangalia maslahi yao, na motisha kutafanya kuvutiwa
na kupenda kuendelea kubaki kufanya kazi
hapa.
“Nikiwa kama Mkuu na mlezi wa bodi hii ya Mkoa huu wa
Mara naihidi kusimamia nakutoa
ushirikiano kikamilifu katika chombo hiki na kiweze kuwa chombo rafiki cha
kufanya nacho kazi.”,alisema Tuppa.
Akizungumzia ujenzi wa hospitali ya kwangwa alisema mkoa huo
tayari umeisha patiwa fedha kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa
kipindi cha fedha cha mwaka 2012/13 ambapo shilingi bilioni 1.5 zimeishaingia
katika mfuko wa hospitali na kwamba hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 38
ambapo mradi huo utajengwa na shirika la Mfuko wa jamii (NSSF) ili uendelee kwa haraka zaidi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Askofu wa dayosisi ya kati Kanisa la Mennonite Amos
Muhagachi alisema wapo tayari kujitolea katika kusimamia utendaji
kazi ili kuleta tija katika kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa.
"Tumepewa
dhamana kubwa ya kusimamia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa
kipindi cha miaka mitatu naamini kwa nguvu za Mungu tutashirikiana na
wajumbe wengine wa bodi hii ili kufikia malengo,"alisema Askofu
Muhagachi
Kwa upande wake Msitahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Alex
Kisurula aliipongeza Wizara ya Afya kwa uteuzi huo na kwamba uanzishwaji wa bodi ni mzuri kwani utaratibu shughuli za
hospitali hiyo ili kupunguza matatizo ya Wananchi.
“Hospitali kwa kupitia bodi kutaweza kufanikisha shughuli
zake kwani bila bodi kunaweza kujisahau na kwenda nje lakini ndani ya bodi hii
huwezi kufanya ubadhilifu,”alisema Kisurura.
Hivi karibuni wagonjwa na wauguzi wamekuwa wakilazimika kununua vyombo kama madishi na majagi kwaajili ya kuhifadhi
mkojo wa waguzi wa wagonjwa hasa nyakati za usiku jambo ambalo walisema linaweza kusababisha milipuko mikubwa ya magonjwa kutokana na baadhi ya wodi katika hospitali hiyo kukosa vyoo.
No comments:
Post a Comment