JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 10/12/2012
Polisi Mkoa wa Dodoma
tumeendelea kufuatilia watu wanaoendesha shughuli za “lambalamba” katika maeneo mbalimbali hususani katika
wilaya za Chamwino, Kongwa na Mpwapwa. Watu hao wanaojifanya kufichua wachawi,
uchunguzi wetu umebaini kuwa wanatapeli watu kwa ajili ya kujipatia fedha.
Pili shughuli wanazoendesha
ni kinyume cha sheria za nchi na ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binanadamu za
kuwaita baadhi ya watu kuwa ni wachawi kwa lengo la kujipatia fedha.
Vitu wanavyojifanya kuvitoa
ndani ya nyumba au maduka ya watu, tumegundua wao wenyewe hutumia baadhi ya
watu kwenda kuviweka / kuvipandikiza na baadaye wanapokuja hujifanya wamevikuta
kwenye nyumba ya mtu anayetuhumiwa kuwa ni mchawi.
Wananchi waelewe kuwa
wanatapeliwa fedha zao na hao watu waliobuni mradi wa kujipatia fedha kwa njia
ya udanganyifu kwani wamejionea wanachangishwa fedha kabla ya kuwaita na hata
wanaodaiwa kuwa wachawi, hudaiwa kiasi cha fedha.
Inasemekana kwamba wanaoendesha
shughuli za lambalamba wanadai pia kutafutiwa wanawake wa kulala nao jambo
ambalo ni hatari kwani mali ya kwamba ni kinyume cha sheria na unyanyasaji wa
kijinsia na pia upo uwezekano mkubwa wa kuambukizwa magonjwa ikiwepo UKIMWI.
Katika kulifanyia kazi
tatizo hilo tarehe 09/12/2012 tumefanikiwa kuwakamatwa watu wane (4) waliokuwa wanajiandaa
kuendesha shughuli za lambalamba katika kijiji cha Vilundilo Wilayani Kongwa.
Watu hao ni:-
1. MKOMBOZI
S/O SALEHE
2. HADIJA
D/O TUPA
3. JOYCE
D/O NHEMBELO
4. SIWEMA
D/O KWAELI
Wanawake hao walikuwa ni
kwa ajili ya kuwapikia lambalamba hao.
Upelelezi unakamilishwa ili
wafikishwe mahakamani wakati wowote. Ufuatiliaji wa lambalamba wengine
waliokimbia unaendelea pamoja na viongozi wanaoshirikiana nao.
Pia Polisi Mkoani Dodoma
inamshikilia kwa mahojiano IDDI S/O RAMADHANI PANDAUYAGA @ NGOSHA, MSUKUMA,
Mkazi wa DODOMA MAKULU baada ya kulalamikiwa na wananchi wengi kwa kujipatia
fedha kwa njia udanganyifu kuwa anawauzia viwanja. Hadi sasa ameshatapeli zaidi
ya Tshs. 24,537,000/= kuanzia mwezi Agosti, 2012. Huwarubuni watu kuwa viwanja
hivyo ametumwa na wafanyakazi wa CDA kuviuza.
Wito kwa wananchi
wasikubali kurubuniwa kuwa wanauziwa kiwanja na kutoa fedha bila kuthibitisha
kiwanja hicho kama kipo na ni halali.
[D. A. MISIME – ACP]
KAMANDA WA POLISI
[M] DODOMA
No comments:
Post a Comment