Monday, October 29, 2012

KONGAMANO LA WANAHABARI NA WADAU WA HABARI MKOANI MARA

 Baadhi ya waandishi na Wadau wa habari wakiwa katika Kongamano  hilo lililoandaliwa na MRPC na MCT
 Mwenyekiti wa Mara Press Club Bw. Emanuel Bwimbo akitoa ufafanuzi juu ya Kongamano hilo
   Shomm B akiwa na Mwenyekiti wa Mara Forum Bw George Chibasa
 Afisa Program Mwandamizi kutoka MCT Bw Astelius Banzi akitoa neno katika Kongamano hilo
    Ahmed Makongo wa Star Tv akiwa mzigoni
 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara Kamishina msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Polisi Abslom Mwakyoma akifafanua jambo katika Kongamano hilo na kupelekea mvutano uliokuwepo na Waandishi wa habari mkoani Mara Kumalizika

 Mdau nikifafanua Jambo katika Kongamano hilo
 Afisa utamaduni Manispaa Mwl Luhende akifafanua Jambo

                             Belensi Alkaid mwakilishi wa Tanzania Daima -Bunda
           Mgeni Rasmi katibu tawala mkoani Mara Bw Clement Lujaji

Waandishi wa Habari Mkoani Mara wameamua kumaliza tofati zao na Jeshi la Polisi baada ya kuweka mgomo wa kuandika Habari kutoka katika Jeshi hilo tangu Septemba 11 Mwaka huu baada ya kuzuia maandamano ya kupinga kifo cha mwana habari Daudi Mwangosi.

Maamuzi ya Kusitisha mgomo huo umetolewa leo kwa kauli moja na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani humo katika mkutano na wadau wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa uwekezaji wa Mkoa wa Mara.

Kamanda wa polisi mkoani Mara kamishina mwandamizi   wa jeshi la polisi Abslom Mwakyoma kupitia mkutano huo amewaomba radhi waandishi wa Habari kwa tofauti zilizojitokeza na kusema kuwa Jeshi hilo linawategemea sana waandishi wa Habari katika kufikisha tofaoti mbalimbali katika jamii.

 Alisema kama ni adhabu waliyotoa Waandishi wa Habari kwa Jeshi la Polisi tangu Septemba 11 wamejifunza na kudai kuwa watahakikisha tofauti zilizokuwepo zinamalizika na kufanya kazi kama timu katika kuisaidia jamii.

Amesema hivi sasa kumeibuka makundi ya wahalifu ya Mbio za vijiti,Mdomo wa furu,Jamaica mocas na G5 ambayo yametishia amani kwa wananchi wa Manispaa ya Musoma na wakati mwingine kusababisha mauji ya raia, hivyo alisema jeshi hilo limejipanga kukabiliana na makundi hayo kuanzia sasa na kueleza bila ushirikiano na Waandishi wa Habari hawawezi kufanikisha.

Kuhusu hatua ya waandishi wa habari mkoani Mara kususia kuandika habari za jeshi la polisi kutokana na kuzuiwa kwa maandamano  hayo,kamanda Mwakyoma,alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kubaini kuwa maandamano hayo hayakufuata taratibu za sheria.
  
Awali katibu tawala mkoa wa Mara Bw Clement Lujaji,akizungumza wakati akifungua mkutano huo,amewaomba waandishi wa habari mkoani Mara kufanya kazi kwa kuzingatia uzalendo pamoja na kuibua fursa zitakazo lenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi  wa mkoa wa Mara.

Alitumia nafasi hiyo,kuliomba jeshi la polisi na waandishi wa habari mkoani Mara,kuondoa tofauti zao ambazo zilijitokeza na kusababisha kususiwa kuandikwa kwa habari za jeshi hilo na hivyo kuwanyima haki wananchi kupata habari ambao ni haki yao ya msingi.

Kwa sababu hiyo waandishi wa habari wa mkoa wa Mara kwa kauli moja chini ya uenyekiti wake Bw Emanuel Bwimbo,walitangaza kuondoa mgomo wa kuandika habari za jeshi la polisi kuanzia sasa na kwamba wamemtaka kamanda wa polisi kukemea unyanyasaji ambao umekuwa ukifanywa na askari wake dhidi ya waandishi mkoani Mara.

No comments:

Post a Comment