WAKAZI WA MARA WASHAULIWA KUACHANA NA TABIA AMBUKIZI
Na Emmanuel Chibasa, Musoma
WANANCHI Mkoani Mara wameshauliwa kuacha tabia ambazo zimekuwa
zikichangia kasi kubwa ya kuongezeko la
maambukizi mapya ya
Virusi vya Ukimwi.
Wito huo umetolewa jana mjini Musoma na
Mratibu wa kitengo cha kuhudumia watu wanaishi na virusi vya Ukimwi CTC
katika hospitali ya mkoa wa Mara Bi Hellen Kure,wakati akizungumza na
waandishi wa Habari ofisini kwake.
Waandishi wa habari wa mkoa
wa Mara waliokuwa kwenye mafunzo ya uandishi wa habari za afya wakiwa
ofisi ya mganga mkuu wa mkoa kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za
afya mkoani humo,mafunzo hayo siku nne yameendeshwa chini ya muungano wa
vilabu vya waandishi wa habari Tanzania(UTPC)yanalenga kuwajengea uwezo
waandishi kuandika habari za afya kwa usahihi
Mratibu huyo wa CTC katika
hospitali ya mkoa wa Mara, alitoa taarifa hiyo juu ya huduma
zinazotolewa na kituo hicho kwa waandishi hao ambao wako katika katika
mafunzo ya uandishi wa habari za afya chini ya ufadhili wa umoja wa
vilabu vya waandishi wa habari nchini UTPC inayofanyika katika ukumbi wa
orange tree musoma.
Akielezea juu ya hali halisi ya maambukizi
ya virusi vya ukimwi tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2004 mpaka
sasa, alisema idadi ya wagonjwa imekuwa ikiongezeka kila kukicha huku
kundi la vijana likiongaza.
Alizitaja sababu kubwa
zinazochangia maambukizi ya ukimwi ni pamoja na kufanya ngono zembe,
wazazi wa kiume kuwa mbali na familia kwa muda mrefu kwa shughuli za
kikazi zikiwemo za uvuvi na uchimbaji wa madini jambo linalowafanya
kujingiza mapenzi mapya.
Hata hivyo Bi Kure,aliesema kuwa kituo
hicho kinapokea idadi kubwa ya watu ambao wamekuwa wakijitokeza kwajili
ya kupima hasa kutoka sehemu mbali mbali za wilaya za Mkoa wa
Mara,huku wengi wao wakiogopa kupima katika vituo viliopo maeneo jirani
na wanapoishi kwa kuogopa kunyanyapaliwa .
Kwa sababu hiyo
alisema hali hiyo imesababisha msongamano wa Wagonjwa katika kituo
hicho,huku akitoa wito kwa Wagonjwa kuacha tabia ya kujinyanyapaa
wenyewe hivyo waendelee kutumia vituo viliopo katika maeneo yao.
“Wakati mwingine pia baadhi ya tabia za watoa huduma za kutoa siri za
wagonjwa zimekuwa zikisababisha wagonjwa kuogopa kupata matibabu katika
maeneo wanayotoka ingawa jambo hili si kubwa sana’alisema mratibu huyo
CTC.
Takwimu za kituo hicho cha hospitali ya mkoa zimeonesha kuwa kuanzia mwaka October mwaka
2004 hadi mwaka 2011 kati ya watu waliojitokeza kupima 43,800 sawa
na asilimia 7.0 walikutwa na maambukizi ya ukimwi na kuanza kutumia dawa
za kuvubaza virusi vya ukimwi.
Kwa mujibu taarifa hizo katika
kituo hicho tu watu 148 wameripotiwa kufariki dunia wanawake 77,wanaume
66,watoto wakike 2 na watoto wakiume 3 ingawa idadi ya vifo inaweza
kuongeka kutokana na ndugu kutotoa taarifa baada ya vifo kutokea
kuhusiana na ukimwi.
Kuhusu changamoto zinazokikabili kituo
hicho alisema ni pamoja na kubadilishwa mara kwa mara kwa watoa huduma
hali inayowaathilipia wagonjwa na utendaji kazi wa kituo kutokana na
mazoea.
“Wanapobadilisha watoa huduma mara nyingi imechangia
wagonjwa kukimbia huduma hata wakati mwingine kushindwa kuendelea na
tiba”aliongeza.
Alitaja changamoto nyingine zinazokikabili
kituo hicho ni pamoja na watoa huduma kubadiliswa wakati wakiwa tayari
wamepata mafunzo maalumu kwajili ya kuwahudumia wagonjwa hao,kukosekana
kwa gharama za mawasiliano kwajili ya kuwakumbusha wagonjwa kuhusu
matumizi ya dawa pamoja na usafiri kwajili ya wahudumu ili kuwatembelea
wagonjwa majumbani.
Kuhusu sababu zinazochangia wagojwa
kukatisha matibabu ni pamoja na kukosa nauli kwajili ya kufata
dawa`katika kituo kwa wale waliombali zaidi jambo linalopelekea wakati
mwingine kuacha kutumia dawa kwa muda muafaka na hivyo kusababisha
usugu na kuhatarisha maisha yao.
No comments:
Post a Comment