MTOTO AZALIWA HANA MIKONO NA MIGUU HOSPITAL YA BUTIAMA
WAKATI Taasisi
mbalimbali zikiendelea na juhudi kuelimisha wananchi kwaajili ya kipinga
vitendo vya ukatili na mauaji ya kinyama wanayofanyiwa watu wenye ulemavu
nchini,mtoto mmoja ambaye amezaliwa bila ya kuwa na mikono na
miguu,yuko katika tishio la kuuawa baada ya baadhi jamii ya kijiji cha Muriaza
kudai kuwa kuendelea kuishi kwa mtoto ni mkosi mkubwa katika kijiji hicho.
Mtoto huyo
ambaye amezaliwa katika hospitali ya Butiama wilaya mpya ya Butiama mkoani
Mara,anadaiwa kuwindwa na baadhi ya watu kwaajili ya kumuua kwa imani potofu
kuwa ni mkosi katika jamii ya kabila la Wazanaki.
Mama
mazazi wa mtoto huyo Bi Maria Joseph,mkazi wa kijiji cha
MURIAZA ambaye ni mwanafunzi kidato cha pili
katika shule ya Sekondari Bumangi,akizungumza
katika hospitalini hapo alipohidhiwa ili kumlinda mtoto huyo,amesema licha
wakazi wa kijiji hicho kutoa tishio pia wachimbaji wa madini wamekuwa
wakimuwinda kwaajili ya kumdhuru kwa imani za kishirikina.
Kwa sababu hiyo
ameomba jamii kumpa msaada kwani hivi sasa analazimika kuishi maisha ya kuomba
omba kwani amedai hata mama ake mazazi amemugopo kutokana na kuzaa mtoto huyo
wanamuita ni KITIMBA kwa jina la kizanaki.
Kwa
upande wake moja ya Madaktari katika hospitali ya Butima Dk Getera
Nyangi,amesema kitaalam tatizo hilo linasababishwa na matumizi ya dawa hasa za
kienyeji ama vitu vya sumu vilivyotumiwa na mama akiwa mjamzito huku
muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo Bi Yohana
Joseph, akidai wamekuwa na kazi kubwa ya kumlinda mama
na mtoto wake na matishio ya mara kwa mara ya watu
wanadaiwa kutaka kumdhuru mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment