MAANDALIZI YA SENSA YAKAMILIKA MARA
MKOA wa Mara umekamilisha
tayari umechukua hatua za haraka za kuhakikisha zoezi la Sensa ya watu na
makazi linafanikiwa kama lilivyopangwa katika visiwa 30 ambavyo vimo ndani ya
ziwa Victoria.
Mratibu wa Sensa
mkoa wa Mara Bw Ramadhan Mbega,amesema mbali na kuyabainisha maeneo hayo pia
imetenga maeneo ya kuhesabia watu katika maeneo ya hifadhi za taifa ya
Serengeti na mapoli ya akiba yanayopakana na hifadhi hiyo.
Amesema kwa mkoa
Mara,maeneo 3335 yametengwa kwaajili ya zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi
ambalo linatarajia kufanyika nchini kote kuanzia Agosti 26 mwaka huu huku kila
halmashauri ikifanya maandalizi ya kufundishia mawakala watakaofanya kazi hiyo.
Hata hivyo Bw
Mbega,amewataka wananchi wa mkoa wa Mara kuachana na dhana potofu ya baadhi ya
watu kuwa endapo watahesabiwa katika zoezi hilo wanaweza kupoteza maisha ama
kushindwa kuzaa.
Bw.Mbega amesema
si kweli kuwa watu wanaweza kuzaa au kupoteza maisha na kuongeza kuwa zoezi
hilo linalenga kuwezesha taifa kupata takwimu sahihi za watu na makazi kwaajili
ya kuwahudumia vema wananchi wake.
Mbali na hivyo
mratibu huyo amempongeza mkuu wa mkoa wa Mara Bw.John Tuppa kwa kuwa mstari
mbele kuhamasisha wananchi kuhusu zoezi hilo la Sensa
No comments:
Post a Comment