Thursday, April 26, 2012

                    MASHUJAA WA MUUNGANO MWALA 1964



Toka kushoto juu ni Bi Sifaeli Choma aliyebeba kibuyu kilichokuwa na udongo  wa Tanganyika na kumkabidhi Mwalimu. Anayefuata ni Bw Omar Hassan Mzee aliyebeba chungu kikubwa ambacho ndicho kilichobeba udongo wa Tanganyika na Zanzibar ambao ulipochanganywa tu ndipo Muungano ukawa umezaliwa, na  kulia ni Bi Khadija Rajab Abbas, aliyebeba kibuyu chenye udongo wa Zanzibar. Mara zoezi hilo lilipokamilika ndipo jina Tanzania likaanza kutumika rasmi. Picha ndogo ya kati inaonesha waasisi wa Muungano wakipita mitaani kusherehekea siku hiyo ya kihistoria, huku wananchi wakiwa wamejipanga barabarani jijini Dar es salaam kuwashangilia wakitokea uwanja wa Uhuru.
 ......................................................................

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete leo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika madhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika katika uwanja wa Uhuru Dar es Salam.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam jana,Bi.Mwamtumu Mahiza alisema kuwa sherehe hizo zitaanza majira ya saa mbili asubuhi ambapo milango ya uwanja huo itafunguliwa kuanzia saa 12 asubuhi.

 ''Sherehe hizi za kiistoria za Muungano zilizo asisiwa na waasisi wetu Baba wa Taifa Julius Nyerere na Hayati Habeid Amani Karume zinatarajia kufana"alisema Bi Mahiza, akiongeza kuwa  viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali watahudhuria  katika sherehe hizo akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Shein. 

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka 48 Serikali imepata mafanikio makubwa ya kujivunia  katika nyanja mbalimbali zikiwemo za maendeleo ya jamii,uchumi,siasa ulinzi,usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa. Kauli mbiu ya mwaka huu ni miaka 48 ya Muungano  shiriki kikamilifu katika sensa na mchakato wa mabadiliko ya katiba.

''Sherehe hizi zitapambwa na gwaride ,halaiki na ngoma kutoka mikoa mbalimbali Tanzania,ambapo pia aliwaomba  SUMATRA na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuelekeza magari yao katika kuelekea uwanja wa Uhuru ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Dar es Salaam"alisema. 

Aliwaomba watanzania kudumisha Muungano kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho wache kusikia maneno ya mitaani kwa kuwa viongozi waliopita wasisi wetu waliomba tudumishe muungano huo. 

Source Michuzi

No comments:

Post a Comment