Thursday, April 26, 2012

Cape Town-Afrika Kusini yasema matatizo ya Afrika yasuluhishwe na Waafrika wenyewe

Afrika Kusini imesema matatizo ya Afrika yanaweza kusuluhishwa na waafrika wenyewe. Hayo yamesemwa jana na waziri wa uhusiano wa kimataifa na ushirikiano wa nchi hiyo Bi Maite Nkosazana-Mashabane alipokuwa akilihutubia bunge.

Bi Nkosazana-Mashabane amezitaka nchi za Afrika kujitegemea katika kusuluhisha migogoro, kupata maendeleo endelevu ya kiuchumi, kuongeza mwingiliano wa kimataifa na kuzidisha biashara kati ya nchi hizo. 

Waziri huyo ametoa wito kwa nchi za bara la Afrika kuinua demokrasia na utawala bora, na kuhakikisha elimu, usalama wa chakula, afya, makazi na ajira vinapatikana kwa watu wote. 

Aidha, Nkosazana-Mashabane amesisitiza nafasi ya Umoja wa Afrika katika kuziongoza nchi hizo kutimiza malengo yake. Ameutaka Umoja huo kujitahidi zaidi katika kuleta maendeleo barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kupambana na umaskini, kutokuwa na usawa pamoja na maendeleo duni.

No comments:

Post a Comment