Thursday, February 16, 2012

MWALIMU AKATWA PANGA ,APORWA FEDHA ZA KIKUNDI

Serengeti
Februari 16,2012.

MWALIMU wa shule ya msingi Majimoto kata ya Busawe wilayani Serengeti
Bhoke Mwita amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na mtu anayedhaniwa
kuwa jambazi na kumkata sehemu mbalimbali za mwili
kwa panga kisha kuchukua tsh,300,000=za kikundi cha kuchangiana.

Tukio hilo la kusitikisha linadaiwa kutokea februari 15,majira ya saa
3 usiku mwaka huu mita chache toka nyumbani kwa mwalimu
,limethibitishwa na polisi na uongozi wa kijiji hicho.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Johannes Masirori aliliambia
gazeti hili kuwa mwalimu huyo alikatwa sehemu mbalimbali za mwili
ikiwemo,shavu la kushoto,mikono ya kushoto na kulia kisha akachukua
fedha hizo na simu na kukimbia.

“Mwalimu ni mweka hazina wa kikundi cha kuchangiana wanawake kiitwacho
upendo alikuwa akitoka kukusanya fedha hizo ili akabidhi
leo(jana)akikaribia kwake ndipo akawekwa chini ya ulinzi na kijana
aliyetambuliwa kwa jina la Magocha Kiring’ani akiomba fedha na
simu”alisema mwenyekiti.

Alisema kabla hajajua nini kimetokea ndipo alianza kumkata maeneo
mbalimbali kwa panga,licha ya kupiga kelele lakini hazikusikika kwa
kuwa kulikuwa na muziki eneo hilo.

“Inaonekana kuwa alikuwa anamfuatilia kwa kuwa baada ya kumweka chini
ya ulinzi kitu cha kwanza alisema anaomba fedha na simu,na kweli
alifanikiwa kuchukua fedha hizo,lakini simu alidondosha na  iliokotwa
na wananchi waliojitokeza baadae”alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo inadaiwa kabla ya kumfanyia unyama mwalimu
alikutana na mama mmoja aliyetajwa kwa jina la Mtabu na kumwamru kukaa
chini,lakini alipomlika akamtambua na kumtaja kwa jina alikimbia na
kwenda eneo jingine ambalo alikutana na mwalimu na kumfanyia unyama
huo.

“Huyo mtuhumiwa anakaa kijiji cha Nyamakhobiti jilani na hapa ,aliwahi
kufungwa kwa uharifu,na baada ya kutoka alikutwa na tuhuma ya ubakaji
akawa amekimbia ,na anaonekana usiku tuna inadaiwa anaishi porini
akijificha ‘alisema.

Alisema jamii kwa kushirikiana na polisi wanamsaka kuhakikisha
wanamkamata kutokana na kukithiri kwa vitendo vinavyohatarisha maisha
ya watu.

Kuhusu hali ya mwalimu alisema baada ya kushonwa majeraha yake katika
zahanati ya Majimoto anaendelea vizuri .

Polisi wilayani hapa wanaendelea na msako wa mtuhumiwa huyo huku
wakiomba jamii ambayo inaishi naye itoe ushirikiano waweze kumtia
nguvuni.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment