Monday, February 27, 2012

HABARI KUTOKA MARA

MUSOMA

KAMPUNI MOJA YA KUCHAMBUA PAMBA NA KUKAMUA MAFUTA YA BIRCHAND OIL MILL YA JIJINI MWANZA, IMEKIRI KUSAMBAZA SEHEMU YA MBEGU ZA PAMBA KWA WAKULIMA WA BAADHI YA MAENEO YA WILAYA SENGEREMA MKOANI MARA AMBAZO ZIMESHINDWA KUOTA KATIKA MSIMU WA KILIMO WA MWAKA HUU.
 
MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI HIYO BW MOHAMED SHARIFF, AMESEMA MBEGU HIZO ZA PAMBA AMBAZO NI SEHEMU YA TANI YA ELFU TANO ZILIZOSAMBAZWA KATIKA MAENEO YANAYOLIMA ZAO LA PAMBA KWA MIKOA YA KANDA YA ZIWA, ZIMESHINDWA KUOTA KUTOKANA NA WAKULIMA WENYEWE KUWEKA MAJI KATIKA PAMBA KWA LENGO LA KUONGEZA UZITO, JAMBO AMBALO LIMESABABISHA PAMBA NA MBEGU ZAKE KUARIBIKA KABLA YA KUREJESHWA KWA WAKULIMA KWAAJILI YA KUPANDWA.

HATA HIVYO AMESEMA TATIZO HILO, IMESABABISHA PAMBA ZAIDI YA TANI MILIONI 7 YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 7 KUHARIBIKA NA HIVYO KUWEZA KUUZWA SEHEMU YOYOTE DUNIANI, HUKU KAMPUNI YAKE IKITOA MBEGU NYINGINE KWAAJILI YA KUPANDA AMBAPO AMETUMIA NAFASI HIYO KUWATAKA WAKULIMA WAFIKIRIE KUTOA FIDIA YA HASARA AMBAYO WAMEISABABISHA KWA WENYE VIWANDA.

TAARIFA ZAIDI ZINASEMA KUWA BAADHI YA MAENEO YANAYOLIMA ZAO LA PAMBA KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA, UMEBAINI KUWA WAKULIMA WENGI WAMEKUWA WAKIWEKA MAJI KATIKA PAMBA KWA LENGO LA KUONGEZA UZITO KWA MADAI YA KUKABILIANA NA WIZI KATIKA MIZANI JAMBO AMBALO LIMECHANGIA KUHARIBU UBORA WA PAMBA.

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

WAFANYA BIASHARA WA SOKO LA MWIGOBERO MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA WAMEITAKA SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA SOKO HILO NA KUIMARISHIA ULINZI KUTOKANA NA UPOTEVU WA BIDHAA UNAOTOKEA MARA KWA MARA KATIKA SOKO HILO.
 
WAKIZUNGUMZA NA KITUO HIKI LEO ASUBUHI KATIKA SOKO HILO, WAFANYABIASHARA HAO WAMESEMA KUWA WANAOMBA UONGOZI WA MANISPA KUBORESHEA MAENEO YA SOKO HILO IKIWEMO KUJENGEWA MEZA ZA KUDUMU KWANI MEZA WALIZONAZO NI ZAWATU BINAFSI NA ZINALIPIWA USHURU KIASI CHA SHILINGI ELFU KUMI KWA MWEZI.

AIDHA MKUU WA SOKO LA MWIGOBERO VEDASTUS MANOTI AMESEMA SWALA LA ULINZI KATIKA SOKO HILO SI WA KURIDHISHA KUTOKANA NA WALINZI WALIOPO KUTOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIKAMILIFU.

AMEONGEZA KUWA KUMEKUWEPO NA WIZI WA BIDHAA NA VIFAA VYA WAFANYABIASHARA KATIKA SOKO HILO KITU AMBACHO KINARUDISHA NYUMA JUHUDI YA KUJIKWAMUA KATIKA JANGA LA UMASKINI.

MKUU HUYO WA SOKO AMETUMIA NAFASI HIYO KUIOMBA MANISPAA YA MUSOMA KURUDISHA ASKARI WALIOKUWEPO KATIKA SOKO HILO BAADA YA KUHAMISHA KWANI INASEMEKANA ASKARI HAO WALIWEZA KUDHIBITI SUALA ZIMA LA ULINZI KATIKA SOKO HILO.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

TARIME

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA UFUNDI SAMARTAN ILIYOKO CHINI YA KANISA LA KIINJIRI LA KIRUTHELI TANZANIA (KKKT) WAMEWALALAMIKIA WALIMU KUWACHAPA VIBOKO VISIVYOKUWA NA IDADI KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO

WAKIONGEA KWA MASIKITIKO NA MWANDISHI WA HABARI HII WANAFUNZI HAO WAMESEMA KUNA BAADHI YA WALIMU WAO WAMEKUWA WAKIWACHAPA VIBOKO MGONGONI NA MIGUUNI WAKATI MWINGINE KUWAPIGA MAKOFI HALI AMBAYO INAWANYIMA FURAHA WAWAPO SHULENI.

BAADHI YA WANAFUNZI WAMEONYESHA KUKATA TAMA KUENDELEA NA MASOMO SHULENI MARA BAADA YA TUKIO LA MWENZAO DAMIAN WA KIDATO CHA PILI KUCHARAZWA VIBOKO VISIVYO NA IDADI PAMOJA NA KUPIGWA MAKOFI BAADA YA KUCHELEWA KUINGIA DARASANI HALI AMBAYO ILIMLAZIMU KUKIMBIA NA KURUKA UZIO WA SHULE KAMA NJIA YA KUJINUSURU.
 
AIDHA WANAFUNZI HAO WAMESEMA KUWA KUENDELEA KUWEPO KWA VIPIGO VIKALI VIMEPELEKEA KUOGOPA HATA KUSIMAMA KUULIZA AU KUJIBU SWALI PINDI WAWAPO DARASANI KUTOKANA NA UWOGA WALIOJENGEWA NA WALIMU WAO.

BAADHI YA WAZAZI WAMEWATAKA WALIMU KUACHA KUWACHARAZA FIMBO SISIZOKUWA NA IDADI KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA KUONGEZA KUWA KITENDO HICHO KINAWAFANYA WATOTO WAZIDI KUWAOGOPA HALI AMBAYO HUWENDA IKASHUSHA KIWANGO CHA TAALUMA AU WATOTO KUACHA SHULE.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

MWANZA.

MKUU WA MKOA WA MWANZA, INJINIA EVARIST  NDIKILO AMEZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA HUO KUHAKIKISHA ZINAJIKITA ZAIDI KUWAHAMASISHA NA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KATIKA SUALA ZIMA LA KUANZISHA MIRADI UFUGAJI NYUKI KWA KILA WILAYA MKOANI HUMO.

MKUU WA MKOA NDIKILO AMETOA MAAGIZO HAYO WAKATI WA ZIARA YAKE YA SIKU MOJA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO KATIKA WILAYA YA MISUNGWI MKOANI MWANZA AMBAPO PAMOJA NA MAMBO MENGINE ALIJIONEA UANZISHWAJI WA MRADI WA KUFUGA NYUKI KATIKA KIJIJI CHA NGUDAMA AMBAPO TAYARI MIZINGA YA NYUKI IMESHAANZA KUWEKWA  KUANZA UFUGAJI HUO.

MKUU WA MKOA HUYO AMESEMA KUWA ANATAKA MKOA WA MWANZA UNAKUWA MFANO WA KUIGWA KATIKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI JUU YA UFUGAJI HUO WA NYUKI HUKU AKIWATAKA MAOFISA NYUKI NA USTAWI WA JAMII WA KILA WILAYA KUACHANA NA TABIA MBAYA YA KUKAA MAOFISINI WAKISUBILI KUPELEKEWA TAARIFA, BALI WAENDE KWA WANANCHI KWA AJILI YA KUTOA ELIMU NA HAMASA HIYO YA KUANZISHA MIRADI YA MIZINGA YA NYUKI.

KWA MUJIBU WA NDIKILO, UFUGAJI WA NYUKI UNACHOCHEA MARADUFU KUINUA VIPATO VYA WANANCHI, KWANI SOKO LA ASALI NA NTA NI KUBWA HAPA DUNIANI, HUKU AKITOLEA MFANO WA AMERIKA KUSINI AMBAPO AMESEMA WANANCHI WA MAENEO HAYO HUKO WAMEPATA MAENDELEO MAKUBWA KWA SABABU YA KUUZA ASALI NA NTA INAYOTOKANA NA UFUGAJI WA NYUKI KATIKA MIZINGA YA KISASA.

AMESEMA AWALI MKOA WA TABORA ULIKUWA UMAARUFU KATIKA SUALA ZIMA LA UFUGAJI WA NYUKI NA UUZAJI WA ASALI NA NTA NDANI NA NJE YA NCHI, LAKINI KWA SASA ASALI YA TABORA IMEANZA KUSHUKA SOKO DUNIANI KUTOKANA NA ULIMAJI MKUBWA WA TUMBAKU AMBAO KIMSINGI NYUKI HUTUMIA MAUA YAKE KUTENGENEZA ASALI YENYE KEMIKALI.

HATA HIVYO, MKUU HUYO WA MKOA WA MWANZA, AMEWATOA WASIWASI WANANCHI JUU YA UPATIKANAJI WA SOKO LA ASALI NDANI NA NJE YA NCHI, NA KWAMBA SERIKALI IPO TAYARI KUANZA KUSAKA MASOKO YENYE UHAKIKA KWA AJILI YA UUZAJI WA ASALI NA NTA DUNIANI.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment