Monday, February 13, 2012

HABARI KUTOKA MARA


Musoma
wananchi wenye hasira kali wa kijiji cha saragana musoma vijijini waliokuwa doria  wamemuua  mwita maseke  kwa kutumia silaha za jadi baada ya kukutwa akiswaga ngombe saba aliowaiba katika kijiji cha buramba wilayani bunda mkoani mara

akithibitisha  kutokea kwa tukio hilo kaimu kamishna wa polisi mkoani mara  acp robert boaz  amesema uchunguzi umeonyesha kuwa marehemu aliiba ngombe hao katika kijiji  cha bulamba na amemtaja mmiliki wa ngombe hao kuwa ni  kasheki lusona

kamanda amesema kuwa katika tukio hilo marehemu hakuwa peke yake bali alikuwa na watu wengine wawili waliofanikiwa kukimbia na haijulikani ni wapi walipoelekea  lakini jeshi la polisi bado linafanya uchunguzi ili kuwabaini watuhumiw hao

kamanda amewataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi wafuate utaratibu kwani wanapofanya hivyo wanapoteza ushahidi na kwamba wanapowakamata wahalifu wawapeleke katika vyombo vya sheria ili wachukuliwe hatua

,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Rorya

madiwani wa halimashauri ya wilaya ya rorya mkoani mara wamewataka wataalamu wa halimashauri  cmt kuwapa majibu sahihi katika kikao cha baraza lijalo juu ya matumizi ya shilingi milioni 51 zilizotumika kujenga barabara ya kilomita 2 kwa madai kuwa pesa iliyotumika ni kiasi kikubwa hakiendani na utengenezaji
wakiongea katika kikao cha  cha baraza la madiwani madiwani hao wameomba ufafanuzi  na mchanganuo wa fedha kutoka kwa wataalamu juu ya kiasi hicho cha fedha lilichotumika kwa madai kuwa kiwango kilichopitishwa  cha utengenezaji wa barabara hiyo inayotoka makao makuu ya wilaya  ingri juu hadi saro kilikuwa ni shilingi milioni 35  lakini badala yake pesa hizo ziliongezeka na kufikia sh.milioni 51.
aidha diwani pita ayoyi  wa kata ya mirare  ambaye pia alikuwa diwani  miaka 5 liyopita amesema kuwa anashangazwa  na cmt kuongeza kiasi cha sh. million 16 ambapo wakati wana vunja baraza  kiwango kilichopitishwa kwa uhalari cha utengenezaji wa barabara kilikuwa sh milioni 35.
kwa upande wake kaimu mhandisi wa ujenzi  julius kahena aliwajibu madiwani hao kuwa barabara haikuwa kwenye bajeti na haukuwepo mpango kazi hivyo kiwango cha milioni 35 kisingetosha barabara ya km 2 kwa sababu  hapakuwa na barabara.
hata hivyo madiwani  hawakulizishwa na majibu hayo ya mhandisi na hivyo kumwagiza  yeye pamoja na  wataalamu wa  (cmt)kufanya upya mchanganuo na kupima upya ili  madiwani hao wajilizishe kilichoongezeka  na namna fedha zilivyotumika.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Tarime
mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya ya tarime mkoani mara fidelis lumato amesema hana kesi na mtendaji wa kata ya matongo deodatus weikama  aliyekamatwa na polisi hivi karibuni kwa agizo la mkuu wa wilaya ya tarime john henjewele.

lumato amesema  kuwa yeye hausiki na kukamatwa kwa mtendaji huyo  na kuongeza kuwa endapo akibainika kutofika kazini kwa mtendaji huyo kwa muda wa wiki mbili atachukuliwa hatua za kinidhamu
awali kukamatwa kwa mtendaji weikama kumekuja baada ya mkuu wa wilaya john henjewele kudai kuwa  ofisi yake imepata malalamiko  ya bi nchagwa kisire (36) kuporwa ardhi na mme wake kisha kushirikiana na mtendaji huyo kufunga nyumba yake januari 23,huku akisababisha mwanae na watoto 3 kuhifadhiwa na majirani
aidha kwa upande wake mtendaji wa kata ya matongo deodatus waikama alipohojiwa na mwandishi wa habari hii mjini tarime baada ya kuachiwa huru na polisi amesema kuwa yeye hakuhusika kufunga nyumba ya bi nchagwa kisire anayelalamika kuporwa kwa ardhi yake  na mme wake ambapo pia alilionyesha vielelezo mbalimbali kuhusiana na malalamiko ya mama huyo.
mtendaji huyo amepinga kauli ya dc ya yeye kushindwa kutatua migogoro ya wananchi hususani malalamiko ya kisire ya uporwaji ardhi ambapo amesema kuwa tayari alikuwa ameshawaita yeye na mme wake ofisini kusuluhisha mgogoro huo baada ya malalamiko hayo  kuyapata kutoka ofisi ya kijiji cha nyangoto.
mbali na hivyo pia amesema  lalamiko hilo alilifikishwa katika  baraza la ardhi na nyumba wilayani tarime baada ya mmewe  kukataa kusuluhushwa kwa kile alichoeleza kuwa yeye ndiye kichwa cha nyumba lazima asikilizwe.
mkuu wa wilaya john henjewele alipotakiwa kutoa ufafanuzi  juu ya  kumuhoji mtendaji  weikama baada ya kuachiwa huru alisema  kuwa mwandishi huyo ataipata taarifa ofisin  kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo .
kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi tarime/rorya jastus kamugisha alipohojiwa juu ya upelelezi unavyoendelea dhidi ya mtendaji huyo kamanda huyo alisema kuwa polisi haiusiki kwani  walitekeleza agizo  kutoka kwa dc.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment