Nimesia kuwa baadhi ya wananfunzi katika chuo kikuu cha Dodoma UDOM watafukuzwa chuo kutokana na kuhusika na mgomo chuoni hapo,ni kweli si sahihi kuweka mgomo katika vyuo vyetu hasa ikizingatiwa serikali inatumia fedaha nyingi katika kugharamia wananfunzi hao.
Kauli yangu kwa viongozi wetu ni kwamba wasitumie nguvu ya madaraka waliyonayo katika kukandamiza watu wengine wasiokuwa na madaraka,tuachanae na hisisa kuwa pengine viongozi wa vyama vyama vya upinzani ndio wanachochea migomo kwenye vyuo vyetu mbona wakati wa Baba wa Taifa migomo ilikuwepo ina maana wapinzani ndiyom walikuwa chanzo? Viongozi wetu msikwepe majukumu yenu kwa kuweka visingizio
Na Mwana wa Afrika
No comments:
Post a Comment