Tuesday, July 5, 2011

DOMINIQUE STRAUSS KAHN MAMBO BADO MAGUMU

Aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa -IMF- Dominique Strauss-Kahn anakabiliwa na mashtaka mengine mapya ya kujaribu kubaka, ambayo yameletwa na mwanamke wa Kifaransa. 

Mawakili wa Tristane Banon, mwandishi wa habari na mtunzi wa vitabu, mwenye umri wa miaka 32 wamesema watamfungulia mashtaka Strauss-Kahn katika mahakama ya Ufaransa, kwa madai ya kujaribu kumbaka mwanamke huyo zaidi ya miaka nane iliyopita.


Akielezea tukio hilo Banon alisema mtuhumiwa huyo alimshawishi kuingia katika nyumba iliyokuwa tupu, akimuahidi kufanya naye mahojiano, kabla ya kujaribu kumbaka. Mawakili wa Stauss-Kahn wamesema mteja wao amekanusha mashtaka hayo na hivyo atamfungulia mashtaka mwanamke huyo kutokana na kumkashifu. Kwa sasa Strauss Kahn anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya New York Marekani, kwa madai ya kutaka kumbaka mhudumu mmoja wa hotel

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment