Mganga mfawidhi wa mkoa wa Mara Dr Wambura alitoa mada katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Halmshauri Musoma Dr Kunei akiwa katika mkutano wa wadau wa afya Tarime leo
Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali mstaafu Enos Mfuru ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo akiwa pamoja na Mganga mkuu wa mkoa wa Mara Dr Samsoni Winani
Mganga mkuu wa mkoa wa Mara Samson Winani akitoa mada katika mkutano huo juu ya kujengwa Kwa hospital ya Rufaa ya mkoa wa Mara ambayo itajulikana kwa jina la MWL NYERERE MEDICAL CENTER ikiwa ni kuenzi mapambano yake katika suala zima la maradhi,ujinga na umaskini katika uongozi wake
Dr Winani akionyesha baadhi ya mchoro wa jengo la hospital ya Mwl Nyerere Medical Center
Kabla ya yote mkuu wa mkoa wa Mara kanali mstaafu Enos Mfuru alifungua mkutano huo ambapo alisema kuwa mkoa wa Mara unachn\angamoto nyingi katika sekta ya afya.Akitaja changamoto hizo alisema ni pamoja na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi ambapo katika wilaya ya Rorya yamepanda sana
Kanali Mfuru akifafanua jambo kwa wajumbe
Hapa mada bado inaendelea
Wajumbe kutoka sehemu mbalimbali ndani nya mkoa wa Mara na nje ya mkoa wa Mara wakisikiliza kwa umakini masuala ya afya yanayojadiliwa katika mkutano huo
Usikivu asilimia 100
Wakuu wa wilaya wakiwa katika mkutano huo,kutoka kushoto ni Fransic Isack wa Bunda na Kanali mstaafu Benedict wa Rorya
Huyu anaitwa George Marato ni mwakilishi wa kituo cha Televisheni cha ITV na Redio One mkoani Mara naye akiwa katika mpangilio wa kuhudhuria mkutano huo ili wananchi waweze kujua nini amabcho wadau hao walijadili katika mkutano huo wa siku tatu.Lengo ni kuhakikisha tunapunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto,maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi na masuala mengine kama ya afya
No comments:
Post a Comment