Wednesday, October 13, 2010

ZITTO ALILIA AMANI MUSOMA

             Zitto Kabwe akihutubia leo wananchi wa Musoma katika viwanja vya Mara Sekondary

MUSOMA
MGOMBEA ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) katika jimbo la Kigoma kaskazini mkoani Kigoma Zitto Kabwe leo amefanya mkutano wa hadahara katika viwanja vya shule ya secondary Mara huku akiwahimiza wananchi kudumiasha amani.
Mkutano huo wa Zitto uliohudhuliwa na Mamia ya wananchi wa jimbo la Musoma mjini ulifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Mara kata ya Nyamatare.
Katika hotuba yake  naibu katibu mkuu huyo wa CHADEMA alisema kuwa kwasasa Taifa letu limegawanyika katika makundi miwili ambapo kuna kundi la matajiri na kundi la Maskini ambao ndio wengi Tanzania.
Alisema waasisi wa Taifa hili walijenga misingi ya upendo na mshikamano kwa watu wote lakini leo kumetokea matabaka ambayo ni hatari kwa taifa lolote lile duniani kwani inahatarisha amani ya nchi
Zitto aliongeza kuwa zamani kipindi cha uongozi wa Mwalimu Nyerere,Karume na Kawawa kulikuwa na shule za serikali ambazo zilikuwa zinakutanisha watoto wa viongozi na wamaskini lakini leo kumekuwa na matabaka ambapo matajiri tayari wamejenga mashule yao na kuyaita Academy.
Alisema shule za kata zimekuwa kero kubwa kwa wananchi kwani hakuna walimu,madawati na vitabu huku viongozi wao wakisomesha watoto wao shule ambazo zina vifaa vyote na hivyo kuweka pengo kubwa la vijana wa Tanzania.
 “Zamani wakati wa Mwalimu Nyerere,Karume na Kawawa kulikuwa hakuna ubaguzi kama huu wa leo unaoletwa na shule za kata,maana motto wa Rais,waziri na maskini walikuwa wanakaa dawati moja lakini leo kitu hicho hakuna bali wameweka shule za watoto wa maskini kitu ambacho si kizuri” alisema Zitto
Mbali na shule pia Zitto alisema kuwa kwasasa hata hospital zipo za matajiri na maskini,ukienda kwenye hospital wanazoita zahanati hakuna na madawa lakini za matajiri kuna madawa.
Naibu katibu mkuu huyo alisema kuwa kwasasa nchi yetu imekuwa na idadi kubwa ya watanzania Maskini kitu ambacho ni hatari kwani ndani ya miaka mitatu maskini wameongezeka kutoka  milioni 11 mpaka milioni 12.9
Akitolea mfano nchi kama Malaysia na Brazil Zitto alisema kuwa Malaysia umaskini umepungua kutoka asilimia 59 mapaka asilimia 53 huku Brazili maskini wakipungua kutoka watu milioni 40 mpaka watu milioni 20.
Akiwanadi wagombea udiwani wa Chama hicho katika kata za manispaa ya Musoma na mgombea ubunge katika jimbo la Musoma, Zitto aliwaeleza wananchi kuwa kama watakipatia Chama hicho ridhaa ya kuwaongoza watahakikisha wanapambana katika kukusanya kodi na kujenga uchumi imara ili wananchi wa Tanzania waondokane na umaskini.
Alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulikuwa na wabunge wachache lakini waliweza kupambana ili mali za watanzanie zitumiwe na wachache,aliongeza kuwa kama watachagua wagombea wa Chadema wana uhakika watafanya vyema kwa miaka mitano ijayo.
Akiongelea amani katika wakati huu wa uchaguzi Zitto alisema kuwa katikakipindi hiki ni vyema watanzania wakawa watulivu kwani amani ndio ngao ya Taifa letu,aliongeza kuwa mataifa mengine yanatucheka lakini wakifika katika suala la amani sisi ndio tunakuwa matajiri na Kiswahili kuwa ngao yetu maana leo nisingeweza kuongea na nyie kama isingekuwa Kiswahili.
  ‘’Ndugu zangu tuwe watulivu katika nyakati hizi za kampuni mpaka uchaguzi maana sisi tunachekwa maskini lakini tukifika kwenye suala la amani mbele ya mataifa mengine sisi ndio tunakuwa matajiri huku Kiswahili kikiwa  kama ngao yetu”
Kuhusu vurugu zilizotokea juzi katika mji huu wa Musoma zitto alisema ni vyema wakuu wa jeshi la Polisi wakafanya uchunguzi wa kutosha na kasha kuwachukulia hatua sitahiki wale wote waliofanya vitendo hivyo ambavyo si utamaduni wa mtanzania,aliongeza kuwa kama amri hiyo  haitatekelezwa leo itatekelzwa pale chama hicho kitakapoingia madarakani.
Akimalizia hotuba yake kwa kuelezea mafanikio ya jimbo lake,Zitto alisema kuwa aliingia katika jimbo la Kigoma Kaskazini kukiwa hakuna Lami katika barabara za huko lakini leo anajivunia katika uongozi wake ameweka Lami kilomita 97.
Alisema kupitia mishahara wake asilimia 30 ameweza kusomesha watoto wa maskini na wasio na wazazi watoto 312 kitu amabcho anasema atazidisha kuanzia mwaka ujao,akimuombea mgombea ubunge kupitia chama hicho katika jimbo la Musoma VIcent Nyerere Zitto alisema kuwa kama wananchi watampatia ridhaa hiyo atasaidiana nae katika kulijenga jimbo hilo na kamwe hawezi kumwacha
 ‘’Mkichagua Nyerere kuwa mbunge wenu kamwe sitamwacha na nitamuonyesha mbinu za kulijenga jimbo la Musoma kama nilivyofanya kigoma’’ alisema mgombea huyo wa kigoma kaskazini
Ujio wa Zitto Kabwe leo katika jimbo la Musoma umesababisha kukosekana kwa watu katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais kupitia chama cha Wananchi (CUF) aliyekuwa anahutubia katika viwanja vya Mukendo mjini hapa.

mwisho

No comments:

Post a Comment