Tuesday, October 12, 2010

KAMANDA BOAZ AKITOA TAMKO JUU YA MATUKIO HAYO


MUSOMA

WATU watano wanashikiliwa na jeshi la Polisi mjini hapa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio lililotokea jana(juzi) ambapo  watu wanaosadakiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi CCM na viongozi wa chama hicho kuhusika katika kuwakata na kitu chenye ncha kali wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kile kilichodaiwa kuwa wananchi hao kutoonyesha ushirikiano na chama hicho tawala.

Wakiongea kwa tabu baada ya kufanyiwa unyama huo katika hospital ya mkoa wa Mara majeruhi hao walisema kuwa kitendo hicho kimetokea jana jioni baada ya mkutano wa kampeni wa cha CHADEMA katika kata ya Buhare.

Sele Mwita(27) ambaye ni mmoja wa wahusika waliojeruhuiwa katika shambulio hilo alisema kuwa wakati anatoka kwenye kampeni za CHADEMA alikutana na kundi la watu wakiwa wamevalia bendera na skafu za CCM huku wakisema kuwa huyu naye anahusika.

     ‘Mimi wakati natoka kwenye mkutano nilikutana na vijana wakiwa na mapanga huku wakiwa wamevaa vitambaa vya CCM wakiongozwa na Kapul na kuanza kusema huyu naye ni wa CHADEMA na kuanza kunikata ndipo nikaanza kukimbia” alisema Sele

Naye Pambano Malima(30) mkazi wa Kigera ambaye mkasa huo ulianzia kwakwe alisema kuwa alikutana na kundi hilo la vijana wakati anapeleka pikipiki na kuanza kumshambulia kwa kumkata mapanga

Walisema kuwa vitendo hivyo vyote vinatokea huku viongozi wa Chama cha Mapinduzi mjini hapa wakiwa wanahusika kwa ukaribu,ambapo mmoja wa kiongozi wa tawi katika kata ya Kigera  Kapul Charles alikamatwa kwa kuhusika na tukio la kwanza la kuwakata vijana wawili mapanga .

Mbali na tukio hilo ambalo limetokea jana usiku lakini leo asubuhi katika kata ya Nyakato mjini hapa wafuasi wengine wawili wa chama cha CHADEMA walivamiwa ndani na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa cha cha Mapinduzi wakisema kuwa washushe bendera zao za CHADEMA ambazo wameziweka katika nyumba zao.

Akiongea na waandishi wa habari mjini hapa leo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi ACP Robert Boaz alikiri kutokea kwa tukio hilo katika eneo hilo la Kigera Migombani.

Alisema kuwa watu waliojeruhiwa walikatwa na vitu vyenye ncha kali baada ya vurugu kutokea ambapo katika eneo hilo kulikuwa na mkutano wa CCM katika nyumba ya Mkono Salima ambaye kamanda Boaz alishindwa kuthibitisha kama alikuwa balozi au la katika hatua hiyo  aliongeza kuwa baada kikao hicho ndipo ulizuka ugomvi huo kati ya vijana waliokuwa ndani na waliokuwa katika maeneo yale.

Akimtaja mmoja wa majeruhi hao ambao waling’ang’aniwa  na mmoja wa aliyekatwa Kapul Charles(42) Kamanda Boaz alisema kuwa  mtu huyo anadaiwa kuhusika katika tukio hilo.

                                     kamanda Boaz


  “Majira ya saa saa mbili kasorobo jana katika eneo la Kigera Migombani kulitokea vurugu ambazo zilipelekea kujeruhiwa kwa watu watatu,inadaiwa kuwa watu hao walikuwa kwenye eneo hilo kwa kiongozi wa kata wa chama cha Mapinduzi” alisema Kamanda Boaz

Kamanda Boaz alisema kuwa kwa sasa kumekuwa na tabia ya wafuasi wa vyama vya siasa kufanya maandamano kitu ambacho hakiruhusiwi katika sheria za uchaguzi za mwaka 2010  na hivyo kusema kuwa ni marufuku kufanya maandamano kwa Chama chochote.

Aidha Kamanda Boaz alisema kuwa uchunguzi wa matukio hayo unaendelea na hakuna mtu yeyote atakayeachwa pale atakapobainika.

Naye mgombea ubunge wa jimbo la Musoma mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA vicent Nyerere  akiongea kwa masikitiko alisema kuwa vitendo hivyo ni vya kusikitisha na si demokrasia katika nchi yetu

Alisema kuwa kulikuwepo na kambi ya vijana wapatao 150 katika shule ya secondary Mshikamano ambao walikuwa wanafanya mazoezi ya kijeshi katika eneo hilo na  katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM,anaongeza kuwa walipojaribu kuuliza kwa uongozi wa jeshi la Polisi habari hizo zilipuuzwa huku katibu wa CCM  akisema kuwa  hao ni vijana wanafundishwa green gurd.

Nyerere alisema kuwa taarifa za uhalifu zinapopelekwa kwa jeshi la Polisi zimekuwa zikipuuzwa na viongozi wa jeshi la Polisi mkoani hapa kitu ambacho kinatia shaka utendaji wa jeshi hilo hasa katika wakati huu wa uchaguzi .

 ‘Tumekuwa tukitoa taarifa kwa jeshi la Polisi lakini tumekuwa tukipuuzwa huku watu hao wakitamba kuwa hawatafanywa lolote na jeshi hilo,hii ni hatari kwa amani yetu’ alisema Nyerere.

Aidha Nyerere alisema kuwa kitendo cha wafuasi hao wa CCM  kuwakata mapanga wafuasi wa CHADEMA kwa kile kinachodaiwa kuwa mtu yeyote anayekutwa amevaa beji ya Dr Slaa na Nyerere.

Mgombea huyo aliongeza kuwa yeye amekuwa akiwindwa na watu wanaosadikika kuwa wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM mjini hapa.

Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mjini hapa hali Ilikuwa shwari lakini ghafla hali hiyo imebadilika kutokana na wafuasi wa vyama vya siasa kuanza kufanya maandamano baada ya mikutano ya Kampeni.


No comments:

Post a Comment