Thursday, February 18, 2016

Jukwaa la BIOTEKNOLOJIA latoa Mafunzo kwa Walimu na Wanafunzi wa Chuo cha BUNDA

Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania na Mkufunzi wa Mafunzo ya Bioteknolojia , Dk. Emmarold Mneney (kulia), akiwafundisha wanachuo wa Chuo cha Ualimu cha Bunda (BUNDA TTC), kuhusu matumizi ya bioteknolojia na uhandisi jeni Wilaya ya Bunda mkoani Mara leo asubuhi.

Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akizungumza na wanachuo hao katika mafunzo hayo.

Wanachuo hao wakifuatilia mafunzo hayo. 


Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Rweyemamu wakiwa katika mafunzo hayo.

Walimu wa chuo hicho wakifuatilia mafunzo hayo.

Wanafunzi wakiwa katika mafunzo.


Wanachuo hao wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.

Mwanachuo, Noshad Bryson akiuliza swali katika mafunzo hayo.

Mwanachuo, Mahana Mahana akiuliza swali.

Mwanachuo, Elias Yohana akiuliza swali.

Hapa baada ya mafunzo ni msosi kwa kwenda mbele.

Na Dotto Mwaibale


JUKWAA la Bioteknolojia Tanzania limetoa mafunzo ya matumizi ya bioteknolojia na Uhandisi Jeni kwa wanachuo cha ualimu Bunda kilichopo mkoani Mara ili kuwa jengea uwezo wa kuielewa teknolojia ya bioteknolojia  kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na changamoto za kilimo.


Akizungumza na wanafunzi hao jana Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk. Emmalord Mneney alisema kuwa teknolojia hiyo mpya ni muhimu kusambaa nchini ili kumkomboa mkulima.

"Tumeamua kuleta mafunzo haya kwa wanachuo hiki tukiamini kuwa baada ya kuhitimu mafunzo yao watakwenda kuwaelimisha wakulima katika maeneo yao"alisema Dk. Mneney.



Dk.mneney aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya tabianchi kumesababisha ukame na uharibifu wa mazingira ambayo yameathiri shughuli za kilimo hasa mazao.


Alisema kuwa kutokana na hali hiyo serikali imekuwa ikiiwezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kwa ajili ya kuwaongezea uwezo wa kufanya tafiti za kilimo nchini.


Dk.Mneney alisema kuwa changamoto kubwa ya wakulima ni kukosa mbegu bora za mazao ya pamba na mahindi hali iliyosababisha wakulima wengi kukata tamaa ya kilimo hicho na kuamua kulima mazao mengine.


"Kutokana na changamoto hiyo Costech imekuwa ikifanya utafiti ndani ya maabara ya kisasa iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ili kupata mbegu bora ambazo zikionekana kuwa zinafaa zitasambazwa katika mashamaba makubwa na nchi nzima kwa ujumla" alisema Dk.Mneney.



Mwanachuo hicho Mahana Mahana alisema mkoa wa Mara unachangamoto kubwa ya kilimo kutokana na ardhi kuchoka hivyo ni wakati wa watafiti kuliangalia hilo ili kuwasaidia wakulima kupata mbegu bora zitakazo waletea mafanikio ya kilimo ya kupata mazao mengi.

Monday, July 27, 2015

Wagombea ubunge ndani ya ccm Musoma mjini waendelea kujinadi kwa wana CCM

MAKADA 9 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameendelea kupita Kata za Jimbo la Musoma mjini kukutana na wanachama wa chama hicho kwenye kampeni ili waweze kuchaguliwa kwenye kura za maoni zitakazofanyika mwishoni mwa wiki hii huku kila mmoja akijitanabaisha kuleta mabadiliko ya kimaisha kwa wakzi wa Jimbo la Musoma mjini iwapo watapiishwa na chama chao kisha kushinda kwenye uchaguzi wa mwezi oktoba        


Docta Musuto Chirangi akiomba kura
Paul Kirigini akiwa na mtoto kwenye mkutano wa kampeni

 Nicodemas Nyamajeje akiomba kura


 kirigini akiomba kura
 Wananchi wa Kata ya Nyakato wakifatilia mkutano wa kampeni

 Mama Maneno akiomba Kura
 Musuto na Juma Mokili ambaye pia ni mgombea wakifurahia jambo

Muuza Dagaa ashinda ubunge viti Maalum Mara

MCHUUZI wa dagaa kwenye mwalo wa Mwigobero uliopo Manispaa ya Musoma,Agnes Methew,ameibuka mshindi wa kwanza kwenye kura za maoni za kutafuta Mbunge wa viti maalumu(CCM) mkoa wa Mara.

Akitoa shukrani kwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa mshindi na msimamizi wa uchaguzi huo,Samwer Kiboye ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya,alisema wajumbe wameonyesha namna ambavyo hata mtu wa chini anaweza kushinda tofauti na inavyozungumzwa.

Alisema wao watu ambao wamekuwa wakizungumza pembeni ukiwa Chma cha Mapinduzi huwezi kupata nafasi ya uongozi kama hauna fedha jambo ambalo sio kweli kwa kuwa yeye amechaguliwa bila kujali kipato chake na kuwashinda walioonekana na kipato cha juu na majina makubwa.

“Niwashukuru sana wajumbe kwa kunipigia kura za kishindo na kunifanya niibuke mshindi kati ya wagombea wengine 9 wanachma wenzangu ambao nilikuwa nikishindana nao ndani ya uchaguzi huu.

“2010 nilikuja kwa mara ya kwanza kuwaomba nafasi hii lakini kura hazikutosha lakini safari hii mmeamua kunichagua mimi muuza dagaa na kuudhilihisha umma ndani ya CCM hata mtu wa hali ya chini anaweza kupewa uongozi.

Kwa jinsi mlivyoniamini naomba   niwahakikishie sito waangusha na kikubwa naomba tupeane ushirikiano na pale nitakapofanikiwa kuingia bungeni nitakuwa mstari wa mbele kuzungumzia masula yanayowahusu wanawake katika kufanikisha chachu ya maendeleo,”alisema Agnes.

Wakati akiomba kura kabla ya kuchaguliwa,mgombea huyo aliwatoa chozi wajumbe baada ya kuomba kura huku akilia akiomba kuchaguliwa muuza dagaa kwa kwa kipindi chote amekuwa yupo na wajumbe katika kiangazi na mvua.

Katika uchaguzi huo,Agnes Methew alichaguliwa kwa kupata kura 418 kati ya kura 641 zilizopigwa na kufuatiwa na Chrstina Samo aliyepata kura 226 huku Mwenyekiti wa (UWT) mkoa wa Mara,Nancy Msafiri akipata kura 208 na kushika nafasi ya tatu.

Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano huo,msimamizi wa uchaguzi,Samwer Kiboye,aliwahasa wagombea wote kukubalina na matokeo kwa kuwa uchaguzi ni wa haki ili kuweza kushirikiana kwa pamoja kutafuta kura za CCM katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba.
 




Sunday, July 5, 2015

Azam TV Yajipanga Kuwapatia Watanzania Matangazo Ya Kihistoria

Azam 6
Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando

Kituo cha Televisheni cha Azam ambacho kina umri wa chini ya miaka
miwili tu sasa kimejipanga kuwapatia Watanzania matangazo ya ubora wa
kiwango cha juu sana wakati wote wa kipindi cha msimu huu wa mchakato
wa uchaguzi mkuu wabunge na Urais mwaka huu wa 2015.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Azam TV Tabata jijini Dar es salaam leo Ijumaa 3 Julai 2015 Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando amesema
“Kwa kuwa tukio hili ni la kihistoria, Azam TV pia imedhamiria kutoa
matangazo ya kihistoria kwa ubora na ufanisi ukilinganisha na aina ya
matangazo ya televisheni ya matukio kama haya katika miaka ya nyuma.
Kwa kutumia teknolojia ya kisasa, vifaa bora pamoja na wafanyakazi
wenye ujuzi na weledi, Azam TV hasa kwa kutumia channel yake ya Azam
TWO, itatangaza matangazo ya uchaguzi wa mwaka huu kwa kipindi chote
cha Uchaguzi kwa kuanzia na harakati za hivi sasa za kutangaza nia kwa
wagombea mbalimbali hasa wale wa nafasi ya Urais kutoka chama tawala
cha CCM na baadaye kambi ya Upinzani.

Azam Televisheni imejipanga kutangaza mfulilizo wa Matangazo ya Moja
kwa moja kutoka Dodoma kwa kutumia vipindi vyake mbalimbali pamoja
na vipindi vingine maalum, pirikapirika zote, harakati zote pamoja na
matokeo yote ya kilele cha mpambano huo wa hatimae kupatikana kwa
mgombea huyo wa Urais wa CCM.
Azam 1
Azam 3 Kutoka kushoto Ni Meb fundi mitambo wa Azam TV, Taji Liundi Mtangazaji na mfanyakazi mwenzao

Tido Mhando amesema “Kuanzia Jumatano July 8 hadi Jumatatu July 13 kikosi cha wafanyikazi wa Azam Televisheni kitapiga kambi Dodoma kueleza kwa kinaga ubaga kila jambo litalokuwa linatokea huko na kwa undani sana ikitumia wachambuzi wenye ujuzi pamoja na kupata na kuzitoa habari za uhakika kwa haraka iwezekanavyo”.

“Matangazo haya yataanzia tangu mapema asubuhi kwenye kipindi chake
cha matangazo ya asubuhi kijulikanacho kama Morning Trumpet, kipindi
maalum cha saa moja wakati wa mchana kuanzia saa saba, kipindi cha
jioni cha Alasiri Lounge, taarifa ya habari maalum ya saa mbili kutoka saa
mbili kamili usiku pamoja na kipindi maalum cha usiku kuanzia saa nne na
nusu hadi saa sita usiku”.

Akiendelea kuongea mbele ya waandishi wa habari Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando Tido Mhando aliongeza kwa kusema “Wakati wa kilele cha hekeheka hizi za huko Dodoma yaani tarehe 11 July na 12 July ambapo mkutano mkuu wa CCM unafanyika, Azam Televisheni itakuwa na matangazo ya moja kwa wakati wote wa mkutano huo na baadae”.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huu, Azam Televisheni itatangaza pia
mikutano na mipango mingine kama hii kwa upande wa vyama vingine vya
kisiasa.
Azam 5
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando

Utaratibu wa matangazo haya ya uchaguzi utaendelea hivi hivi wakati wa
kipindi chote cha kampeni kuanzia mwezi wa August hadi tarehe yenyewe
ya uchaguzi hapo Octoba 25.

Labda ni wakati wa kipindi hicho cha uchaguzi kamili ambapo Azam
televisheni imejiimarisha zaidi kuweza kuwapatia watazamaji wake
matangazo bora ya kisasa zaidi kuliko wakati wowote katika historia ya
utangazaji nchini hapa.

Kwa kuzingatia umuhimu wa uchaguzi na upatikanaji wa habari za uhakika
kwa watanzania Azam imeweka dhamira hii kama sehemu ya historia kwa
kutimiza wajibu wa msingi wa vyombo vya habari kwa umma wa
watanzania.

Kwa kutumia studio bora kuliko zote karika kanda hii ya Afrika pamoja na
vifaa vingine vya kileo kabisa, Azam televisheni itatangaza mfulilizo na
moja kwa moja matukio yote muhimu ya wakati huo wa kupiga kura,
kuhesabiwa kwa kura na hatimae kutangazwa washindi wa nafasi ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar, Wabunge wa bunge la
Muungano na Baraza la wawakilishi, Zanzibar.

Kujiamini huku kwa Azam Televisheni katika kutekeleza lengo hili kubwa
kunafuatia kuajiriwa kwa kundi la watangazaji mahiri ambao kwayo ujuzi na
uelewa wao pamoja na misingi ya weledi itakayozingatiwa bila ya shaka
utawezesha ari hii kutekelezwa kwa kiwango cha mafanikio makubwa.
Miongoni mwa watangazaji hao ni Charles Hilary, Ivona Kamuntu, Fatuma
Nyangassa, Baruani Muhuza, Hassan Mhelela, Faraja John, Raymond
Nyamwihula, Jane Shirima, Phillip Cyprian, Mwanga Kirahi, na Taji Liundi.
4
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando

Tuna amini ya kwamba kundi la watangazaji hawa wenye ujuzi na wengine
wachache ambao watakuja hivi karibuni wakiungana na wale vijana
wasomi ambao tayari wamekuwepo wataweza kufanikisha ile ari ya
kukifanya kituo cha Azam Televisheni kuwa bora zaidi katika kanda hii.
Mbali na kuimarishwa kwa kitengo cha habari lakini mipangp na mikakati
bora imeandaliwa ya kupata vipindi vingine bora vya aina mbalimbali
ambavyo vitatayarishwa kwa kiwango cha juu na cha hadhi ya kimataifa
ikiwa ni pamoja na kuimarishwa kwa kiasi kikubwa kwa matangazo ya
vipindi vya michezo na matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu
ikiwa ni pamoja na yale ya ya ligi kuu ya kandanda Tanzania yaani
Vodacom Premier League.

Kwa kuwapatia watazamaji wetu na watanzania kwa ujumla matangazo
haya bora ya vipindi vizuri vya televisheni, tunauhakika wanunuzi wa
ving’amuzi vya Azam watakuwa wanapata wakitakacho na zaidi.

Tuesday, June 9, 2015

Picha mbalimbali kutoka Musoma wakati Prof Muhongo akitangaza nia ndani ya CCM kugombea urais wa Tanzania

            Profesa Sospeter Muhongo akielezea umati ulioko mbele yake sababu ya kuomba nafasi hiyo
                              Wazee wa mkoa wa Mara wakimsikiliza Prof Muhongo
                              Ukumbi ulishiba ikabidi wawe hadi nje
                                                Makundi mbalimbali yalikuwepo
                              Matangazo hayo yalikuwa moja kwa moja kupitia AZAM TV na CH 10
                                  Burudani kwa wote hawakulala na mambo yakawa poa
                  Baada ya kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa jamaaaa haooo Kenya