SERENGETI.
MAHAKAMA ya Hakimu wa Wilaya ya Serengeti
imelazimika kuhamia hospitali ya wilaya ya Nyerere na kumsomea mashitaka Marwa Ibrahimu(30)mkazi wa Kijiji cha Matare
wilayani hapo,anayekabiliwa na mashitaka mawili ya kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 12.
Hakimu wa Mahakama hiyo Franco Kiswaga
alilazimika kuhamia hospitalini hapo kutokana na mtuhumiwa kushindwa kufikishwa
mahakamani kufuatia kupigwa na kuumizwa na wananchi walipomkuta anafanya unyama
huo .
Mwendesha mashitaka wa polisi Jakobo Sanga
akisoma maelezo ya shitaka hospitalini hapo alisema mnamo novemba 19 mwaka huu
majira ya saa 2 usiku katika kitongoji cha Bukore kijiji cha Nyichoka kata ya
Kyambahi mtuhumiwa anadaiwa kumbaka na kumlawiti mtoto wa miaka 12.
Akisoma hati ya mashitaka alisema kuwa
mshitakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili ikiwemo la ubakaji na kulawiti
mtoto kinyume cha maumbile ikiwa ni kinyume cha sheria.
Na kuwa mtuhumiwa akijua kuwa ni kosa
alimkamata mtoto huyo na kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia majeraha sehemu
za siri na haja kubwa mtoto huyo.
Mwendesha mashitaka alisema kuwa upelelezi
umekamilika,hata hivyo mshitakiwa alikana mashitaka na hakimu kuamru apelekwe mahabusu
atakapopona hadi desemba 5 mwaka huu
kesi hiyo itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment