Ghati Mikere akiuguza majeraha
Mratibu wa dawati la polisi la Jinsia WP Sajenti Sijali Nyambuche akichukua maelezo ya Ghati walipotembelea majeruhi mbalimbali hospitalini hapo
Serengeti:
WAKATI wadau
mbalimbali kwa kushirikiana na serikali wakiwa katika kampeini za kupinga
vitendo vya ukatili wa kijinsia,Ghati
Mikere(20)mkazi wa Kijiji cha Bisarara wilaya ya Serengeti amenusurika kufa
kufuatia kukatwa shingo na sikio baada ya kukataa kufanya ngono na shemeji yake .
Tukio hilo
lililompelekea kulazwa wodi ya wanawake hospitali ya wilaya ya Nyerere limethibitishwa
na polisi na uongozi wa hospitali,linadaiwa kutokea novemba 30 mwaka huu majira
ya saa 5:asubuhi nyumbani kwa majeruhi huyo.
Akiongea kwa kugugumia
kutokana na maumivu akiwa wodini alisema
shemeji yake Chacha Kitari alimkata baada ya kukataa kushiriki tendo la ngono
kwa madai ya kuondoa mkosi wa mme wake kufungwa jela ,alipokataa ikapelekea
kukatwa sikio la kushoto na shingo.
“Kabla ya
kunishambulia kwa fimbo na kunikata kwa sime…alinitaka nifanye naye ngono kwa
madai kuwa ni maamzi ya ukoo na itasaidia kuondoa mkosi kwenye ukoo…kisha
amiliki mji na ndiye awe mme wangu ..yaani wameishajipanga kama mme wangu
anafia huko”alisema kwa masikitiko.
Hata hivyo Ghati
hakuwa tayari kusema mme wake kafungwa miaka mingapi na kwa kosa lipi,na
ameanza kutumikia kifungo lini.
Alisema licha ya
kupiga kelele kuomba msaada ,ndugu walimpuuza na ndipo akapata msaada kwa
majilani wa kufika hospitali kwa kupitia polisi.
Mkuu wa kituo
cha Polisi Mugumu ASP Joseph Maganga ambaye aliongoza dawati la jinsia akiwa
hospitalini hapo alisema ,wanaendelea kumsaka mtuhumiwa kwa kuwa matukio ya
ukatili wa kijinsia yameshamiri na kuomba jamii kutoyafumbia macho kwa kuwa
madhara yake ni makubwa kwenye familia na taifa.
Katika tukio
jingine mwanamke mmoja Mgosi Chacha (20)
mkazi wa mtaa wa bomani mjini Mugumu naye amelazwa hospitali baada ya
kujeruhiwa vibaya na mme wake wa kufikia kwa madai ya kukataa kurudisha mahari iliyotolewa na mwanamke
aliyemuoa(Nyumba Nthobu).
Akiwa wodi la
wanawake mbele ya dawati la jinsia la polisi alisema desemba 2.majira ya saa tatu usiku mwaka huu akiwa nyumbani
kwake mtaa wa bomani mwanamme huyo Chacha Charles mkazi wa kijiji cha Bonchugu alimfanyia
unyama huo baada ya kudai hatarudisha mahari ya mwanamke huyo kwa kuwa aliolewa
kwa mila na desturi za Kikurya.
“Nimeolewa kwa
ng’ombe 12 kutoka kwa bibi Bhoke Charles …ndoa ya Nyumba Nthobu…huyo mwanamme
yeye ameteuliwa na ukoo wa bibi ambaye alinitolea mahari…ambaye hakuzaa na
ameishakuwa marehemu …amenizalisha watoto wanne ambao ni mali ya alinitolea
mahar”alisema.
Alisema siku
ya tukio Charles akiwa nyumbani
mtuhumiwa huyo alifika na kusema anataka ng’ombe hao kwa kuwa amemweleza muda mrefu
bila utekelezaji,na kumpa nafasi ya kujibu na alianza kumshambuli na kumjeruhi
sehemu mbalimbali za mwili,kana kwamba haitoshi alimchukuakua usiku huo akiwa
ajitambui na kwenda kumtupa kwenye shimo refu umbali wa kilomita 2 kutoka
nyumbani kwake ambapo aliokotwa asubuhi na wapita njia ambao walitoa taarifa polisi na yeye alipata fahamu na
kujikuta amelazwa hospitali.
“Kwa sasa hali
za wanawake hao zinaendelea vizuri na wanapata huduma ya matibabu , tofauti na mwanzo walipofikishwa Hospitali
walikuwa katika hali mbaya”,alisema Musa
Wilison Muuguzi mwandamizi msaidizi .
No comments:
Post a Comment