Baadhi ya
wakazi wa Mkoa wa Mara wametoa pongezi kwa Waandishi wa habari waliofanikisha
kukamatwa mtu aliyekuwa akijitambulisha katika idara mbalimbali za Serikali
kuwa ni Afisa usalama kutoka Makao Makuu.
Wananchi
hao walisema kuwa kitendo cha Mtu huyo kuwasiliana na Mkuu wa mkoa wa Mara na
kuagizwa kwa baadhi ya Maafisa waandamizi wa vyombo vya usalama kuambatana nae
kwa kile alichokuwa akidai kuwepo kwa mtandao wa watu wanaosafirisha risasi
bila kumshtukia ni cha hatari katika
suala zima la usalama
“Hili
tukio ni la kushtua sana maana mtu huyu amedanganya Mkuu wa mkoa na baadhi ya
wakuu wa vyombo vya usalama bila kumshtukia na mpaka wanampatia sehemu ya
kulala na chakula bila kutumia mbinu zao kumgundua ni hatari sana” alisme bw
John Magafu mkazi wa Nyamatare.
Bw Liso Chacha - Afisa usalama feki
Katika
hatua nyingine Bw Samson Chacha Mkazi wa Bweri Manispaa ya Musoma Mkoani Mara alisema
kuwa kitendo hicho kimewatia shaka katika suala la usalama na hivyo kuvitaka vyombo vya
usalama kuongeza umakini.
Alisema wakati
mwingine baadhi ya idara za Serikali zinaona
waandishi kama adui na kushindwa kuwapa ushirikiano jambo ambalo halipaswi
kufumbiwa macho kwani kitendo kilichoonyeshwa na baadhi ya waandishi kumshtukia
Afisa huyo feki ni cha kishujaa na kuonyesha wapo mstari wa mbele katika
kuilinda nchi yao.
‘Mimi
nawapongeza sana hawa waandishi maana
wameonyesha kitendo cha kishujaa sana
maana haiwezekani siku karibia tatu mtu huyo anacheza na akili za watu wenye
dhamana ya ulinzi katika Mkoa mpaka waandishi ndiyo wamshtukie” alisema Bw
Samson
Julai 17
Bw Liso Chacha alifika katika ofisi za ITV mkoani Mara na kuwakuta waandishi wa
habari wa Channel Ten (Augustine Mgendi) na ITV (George Marato) ambapo alidai
kuwepo kwa mtandao wa watu wanaovusha risasi kutoka kikosi cha 27 KJ Makoko na
hivyo kuhitaji msaada wa waandishi hao katika kufanikisha lengo lake la
kuwakamata watu hao.
Katika
kujitambulisha kwake Bw Liso alisema kuwa ni Afisa usalama kutoka Makao Makuu
na hivyo yupo mkoani Mara kwa Kazi Maalum
jambo ambalo lilitiliwa shaka na Waandishi hao pale walipomuuliza Makao
makuu ya Usalama wa Taifa nchini yapo sehemu swali ambalo alionekana kushindwa
kulijibu.
Kufuatia
hatua hiyo Bw Liso alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mara kutokana na taarifa
zilizotolewa Polisi na waandishi hao ambapo taarifa hizo ndizo zilizowashtua
viongozi mbalimbali ambao tayari walikuwa wamemuamini Bw Liso kama Afisa
Usalama kutoka Makao Makuu.
Baada ya
Ushahidi kutolewa na mashahidi saba akiwemo Afisa utumishi kutoka idara ya
usalama wa Taifa,Desemba 4 hukumu ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya
ya Musoma Bw Richard Maganga, ambapo alisema kuwa Mahakama imeridhishwa na
Maelezo ya Mashitaka wakiwemo mashahidi saba kutoka idara mbalimbali ambazo ni
Jeshi la Polisi,Mkuu wa utumishi idara ya usalama wa Taifa ,Waandishi wa
habari na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na hivyo kumtia hatiani mtuhumiwa huyo
kwa kujifanya Mtumishi wa idara ya Usalama wa Taifa na hivyo kwenda jela Miaka
mitatu
No comments:
Post a Comment