MUSOMA
Baadhi
ya Walemavu katika Manispaa ya Musoma
mkoani Mara wameomba kushirikishwa
katika Vikao mbalimbali vya Maamuzi Mkoani humo kama njia ya Kupanga na kushauri
mambo yanayowahusu watu wenye ulemavu
katika Maisha yao
ya kila siku.
Mwenyekiti
wa Chama cha Walemavu wa Viungo Mkoa wa Mara (CHAWATA) Bw Yohana Magai katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho ambao
ulikuwa ni Maalum kuchagua viongozi wa Chama hicho.
Mwenyekiti
huyo pia aliomba kutengwa kwa fedha ambazo zitasaidia kuendesha mambo
mbalimbali yanayowahusu na kuwepo takimu sahihi za watu wenye ulemavu hapa
nchini ambapo kwa Mkoa wa Mara idadi ya Walemavu wa Viungo ni 8,856.
“Nasi
tunapaswa kupewa Mafungu ambayo yatatusaidia katika kuendesha shughuli zetu na
kujua takwimu sahihi za Walemavu hapa nchini na kwa kufanya hivyo naamini
Serikali itajua jinsi gani ya kutusaidia” alisema Mwenyekiti Magai
Akisoma
Taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za CHAWATA Mkoa wa Mara kwa kipindi cha
miaka Mitano 2008-2013 Katibu wa Chama
hicho Bw Leonard Lameck alisema kuwa katika kipindi hicho Chama kimeweza kuwa
na Ofisi kwani hilo
lilikuwa tatizo kubwa tangu kuanzishwa kwa Chama hicho Mwaka 1982.
“Kutokuwa na ofisi ilikuwa ni Changamoto
kubwa kwa Chama chetu lakini tunashukuru tangu tumeingia Madarakani tumeweza
kufanikisha kupatikana kwa ofisi nah ii ni tangu kuanzishwa kwa chama hiki
mwaka 1982: alisema Katibu huyo.
Baadhi ya Wajumbe katika Mkutano Mkuu wa CHAWATA MARA
Pamoja na
Taarifa hiyo kuonyesha Mafanikio katika kipindi cha Miaka mitano lakini pia
Chama hicho bado kinahitaji Msaada mkubwa katika kuendeleza kazi za Chama hicho
ikiwemo kuelimisha Jamii ya watu wenye ulemavu.
‘Bado tuna Matatizo makubwa sana katika Chama chetu ili tufikie Malengo
lazima tupoate wafadhili mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi”alisema Bi
Leonard
Changamaoto
nyingne ambazo zilielezwa katika taarifa hiyo ni pamoja na kutokuwepo kwa vyanzo
vya Mapato,ukosefu wa kadi za Wananchama,ukosefu wa vyenzo vya kujongea na vifo
ambapo katika kipindi cha Miaka mitano viongozi watano wa CHAWATA Mara
walifariki duni kutokana na magonjwa mbalimbali.
Akifungua
Mkutano huo Bi Magreth Munduli ambaye ni
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mara aliwataka Watu wenye ulemavu kufanya kazi
kwa ukaribu na ofisi za Serikali ili wasione kama
wanabaguliwa katika Mambo mbalimbali ya Maamuzi
Alisema
watu wenye ulemavu wamekuwa na Changamoto nyingin lakini wao kama
watendaji watajitahidi kuwasaidia ili wawe katika Mazingira bora.
“ Tunajua Mnachangamoto nyingi lakini kama
ofisi tunajitahidi kupambana nazo ili msione kama
mnabaguliwa lakini pia andikieni Maandiko yetu na mmpelekee Mkurugenzi ili
bajeti ikiwa inapangwa nanyi mtazamwe” alisema Bi Magreth Mundulu
Katika
Mkutano huo wanachama walimchagua Bw Yohana Magai kuendelea na nafasi ya
Mwenyekiti na Leonard Lameck nafasi ya Katibu huku nafasi wa Mweka hazina
ikienda kwa Lucyiana Daudi ambapo watakaa katika nafasi hizo kwa kipindi cha
Miaka mitano
No comments:
Post a Comment