Vijana nchini wametakiwa kujihusisha na shughuli
mbalimbali za uzalishaji Mali
katika kujipatia kipato ikiwa ni njia ya kuepuka kutumiwa na baadhi ya wanasiasa
kutimiza Malengo yao.
Kauli hiyo ilitolewa na Umoja wa Vijana wa Chama cha
Mapinduzi UVCCM wilaya ya Butama mkoani Mara katika baraza la Vijana la wilaya
hiyo lilofanyika Butiama mkoani hapa.
Bwana Gerald Joseph. Mwenyekiti wa VCCM. Butiama Bunda Mara |
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Butama mkoani Mara Bw Gerald Joseph alisema Vijana wilayani humo wamefia hatua ya kufanya Siasa na Uchumi kama njia ya kujikwamua katika lindi la Umaskini na kuepuka kutumiwa na baadhi ya wanasiasa.
" Tumeamua kufanya Uchumi na siasa na hii itatusaidia kuepuka kutumiwa na baadhi ya wanasiasa ambao Mara nyingi huwatumia vijana na Mwisho wa siku kijana hubaki bila msaada" alisema Mwenyekiti huyo
Katika kufanya siasa na Uchumi Mwenyekiti huyo alisema kuwa vitega uchumi mbalimbali vitaanzishwa katika mikakati ya kujikomboa kiuchumi aambapo sehemu kubwa watajikita katika kilimo na ujenzi wa hostel za kupangisa.
Katika
hatua nyingne baadhi ya Vijana ambao ni wajumbe katika Baraza hilo
waliwaasa vijana wenzao kutotoa mwanya kwa wanasaisa kuwatumi
bali wajipange katika kufanya siasa na Uchumi kama
njia ya kutokuwa ombaomba.
Walisema kutofanya hivyo wataendelea kuwalalamikia Viongozi kuwa wanawathamini hasa nyakati za uchaguzi jambo ambalo walisema wanalipinga.
" Lazima tujitegemee sisi wenyewe hasa kwa kufanya siasa na Uchumi kuliko kuwategemea wanasiasa ambao dakika ya mwisho baada ya kufanikiwa hatuwaoni" alisema Julius mmoja wa wajumbe wa baraza hilo

No comments:
Post a Comment