Serikali imetakiwa kuchukua hatua za haraka ambazo zitasaidia kukabiliana na
tatizo la njaa katika wilaya ya Serengeti Mkoani Mara lililosababishwa na ukame
pamoja na uvamizi wa tembo katika baadhi ya maeneo ya Makazi ya watu na
Mashamba.
Baadhi ya Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoani Mara walitoa kauli hiyo katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ambapo suala hilo lilionekana kutumia muda mrefu katika kulijadili.
Mkurugenzi halmshauri ya Musoma kushoto na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Ng'oina.
Walisema kumekuwepo na tatizo la njaa katika wilaya
hiyo ambalo limesababishwa na Ukame lakini pia kuwepo kwa tembo
wanaoingia katika Makazi ya watu na Mashamba na kufanya uharibifu wa Mazao
katika Mashamba jambo ambalo limesababisha tatizo kubwa la njaa.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Bw John Ng'oina alishauri kuwepo kwa uzio katika maeneo ya hifadhi huku Mkurugenz wa Halmashauri hiyo Bi Goody Pamba alihimiza kulima mazao yanayokomaa haraka na Wafugaji kuuza baadhi ya Mifugo na kununua Chakula.
No comments:
Post a Comment