Friday, November 15, 2013

RC MARA AMALIZA MGOGORO WA DC NA MBUNGE RORYA

Mbunge wa Jimbo la Rorya Mh Lameck Airo na mkuu wa wilaya Elias Goroyi wamekubaliana kuweka tofauti zao pembeni na kujumuika pamoja katika suala la maendeleo ambalo lilikuwa limesimamishwa na uhasama baina yao.



Uhasama huu ulijikita katika maswala ya siasa na shutuma za ushirika wa viongozi hawa katika wizi wa mifugo umemalizwa na mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa akishirikiana na baadhi ya wazee na viongozi wa dini.

Viongozi hao ambao ni mkuu wa wilaya ya Rorya Elias Goroyi na mbunge wa jimbo hilo Lameck Airo kwa pamoja na mbele ya kikao kilicho itishwa na mkuu wa mkoa mara Bw John Gabriel Tupa katika mji mdogo wa utegi na kushirikisha wazee maarufu wa wilaya Rorya na viongozi wa madhehebu ya dini viongozi hao wameondoa tofauti zao. 

Kitendo cha viongozi hao kukubaliana na kuondoa tofauti zao kimepongezwa na wazee na vingozi wa dini na kuwataka waliyo yasema yawe yametoka moyoni mwao kama walivyo tamka wenyewe.

Mzee Kembo Migore akiwakilisha baadhi ya wazee waliokuwepo katika Mkutano huo alisema kuwa kinachotakiwa viongozi hao ni kukaa pamoja na kusukuma gurudumu la Maendeleo mbele.

"Mkuu wa Mkoa umefanya jambo jema sana sisi tunachotaka ni kupeleka gurudumu mbele hivyo DC na Mbunge mshirikiane " alisema Mzee Kembo

Nao baadhi ya Viongozi wa dini walioshiriki katika Mkutano huo walihimiza amani na upendo miongoni mwa Viongozi hao ambapo walisema bila Amani hakuna Maendeleo
Akifunga kikao hicho mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa ametoa wito kwa viongozi wote wa mkoa mara wawe na tabia ya kuwa na vikao vya mara kwa mara vitakavyo wasaidia kubaini baadhi ya changamoto zinazo wakabili na kuzitatua kwa wakati bila malumbano.

No comments:

Post a Comment