Muheshimiwa Waziri
wa Maliasili na Utalii Kahasheki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
matembezi ya amani ya Tembo Duniani kupinga mauaji ya Tembo hao.
Muheshimiwa Waziri
wa Maliasili na Utalii Kahasheki akionesha moja ya vibao ambavyo
vinawaonesha Tembo wakati wa Matembezi hayo ya amani.
Kutoka kushoto ni
Mrs. Tibaijuka akifuatiwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii
Kahasheki,Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Willbert
Chambulo, na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Muheshimiwa Magesa Mulongo.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa katika Matembezi ya Siku ya Tembo Duniani
Baadhi ya Wanaharakati wakiwa katika Matembezi ya siku ya Tembo Duniani
Ma elfu ya
Wananchi kutoka Arusha pamoja na wadau wengine kutoka Mikoa na nchi
mbalimbali wakiwa katika Matembezi ya siku ya Tembo Duniani yaliyo
Fanyika Arusha Leo
Hawa ni Watoto Shupavu kabisa waliojitolea Mstari wa mbele katika Matembezi ya Tembo leo
Muheshimiwa Waziri
wa Maliasili na Utalii Kahasheki akisaini katika moja la bango la siku
ya Tembo , ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu
Maandamano yakiwa yanaendelea
Wa kwanza kutoka
kushoto ni Mr. Peter ambaye ndiye alikuwa katika kamati kuu ya
Maandalizi ya Siku ya Matembezi ya Tembo Duniani, na pia Makamu
mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours operators akiwa katika
matembezi hayo
Muheshimiwa Waziri
wa Maliasili na Utalii Kahasheki akiongoza Ma elfu ya watu wakiingia
katika viwanja vya AICC ambapo ndipo ilikuwa kilele cha Matembezi hayo
Afisa Mtendaji wa
Chama cha Wakala wa Utalii TATO Ndugu Sirili Akko akitoa Maneno machache
kabla ya ufunguzi Rasmi wa Kilele cha Matembezi ya Tembo Duniani.
Meza kuu
wakiongozwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki wa
nne kutoka kushoto wakiwa wamesimama kwa mda wa dakika moja kuwakumbuka
Waliokufa katika Tukio la Westgate Kenya pamoja na Tembo walio uwawa .
Mc akiwa anaanza Tukio rasmi kwa kuwakaribisha viongozi mbalimbali kwa ajili ya Kutoa salam zao na Risala
Dr. Alfred kikoti
Akitoa Mada yake juu ya Idadi ya Tembo ambao wamebakia , pia kuelezea
kutokomeza kwa Biashara haramu ya uuzaji wa uuzaji wa Meno ya Tembo, na
kusisitiza Tanzania inategemea Tembo katika Utalii.
Mwenyekiti wa
Tanzania Association of Tours Operators Ndugu Wilbert Chambulo akielezea
juu ya kusimamisha biashara kubwa ya Meno ya tembo ambayo inaongozwa na
Nchi ya China na kuziomba Nchi zengine kusimamisha Biashara hiyo Haramu
.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Mongela wa Arusha Akimkaribisha Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Muheshimiwa Magesa Mulongo akiwashukuru wananchi wa Arusha kwa
kushiriki kikamilifu zoezi la matembezi ya siku ya Tembo Duniani na
kumkaribisha Mgeni Rasmi Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii
Kahasheki kutoa hotuba yake.
Muheshimiwa Waziri
wa Maliasili na Utalii Kahasheki akizungumza na wanaharakati waliofika
katika siku ya Matembezi ya Tembo Duniani, kwa kutoa Salamu kutoka kwa
Muheshimiwa Rais Kikwete kwamba Oparesheni ta kutokomeza majangili
imeanza na Haitasimama, alisisitiza kwamba Wanasheria wafunge midomo yao
kuhusu kutetea haki za binadamu , Aliongeza kwamba majangili wauwawe
huko huko wakikamatwa kurahisisha msongamano wa kesi mahakamani, na
Mwisho aliongeza kwamba Wanasiasa wasiingilie swala hili la kupambana na
ujangili.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akikabidhi vyeti kwa Shule Zilizo Shiriki Katika Matembezi ya Tembo Duniani
Muheshimiwa Waziri
wa Maliasili na Utalii Kahasheki akipokea zawadi kutoka kwa TATO Anaye
mkabidhi zawadi hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa TATO Mr. Peter
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mlongo akipokea zawadi kutoka TATO Anayemkabidhi ni Bi. Tibaijuka
Mkurugenzi mkuu wa
Hifadhi za Taifa Ndugu. Allan Kijazi akitoa neno la Shukurani wakati wa
kufunga Kilele cha siku ya Matembezi ya Tembo Duniani leo
Hawa ni Wale
waliotembea katika Matembezi ya Kupinga mauaji ya Tembo Kutoka Arusha
hadi Dar es salaam Mwendo wa Kilometa 650 kwa Siku 12 Kutoka kushoto ni
Binti Mdogo mwenye umri wa Miaka 20 Kaptorina Manange,Mkazeni Y.
Mkazeni, Rehema Y. Najema, na Livingstone Y. Mkazeni.
Maandamano haya
yalitokea Jirani na Cultural Heritage Hadi Viwanja vya AICC Kijenge
Jijini Arusha, Matembezi yaliyo andaliwa na Tanzania Association Tours
Operators (TATO)
No comments:
Post a Comment