BIDHAA MPYA GHARAMA NAFUU FIKA DUKA LA TIGO MUSOMA
Bi Pilila Kavishe
HAPA KAZI TU
ZAWADI KW WATEJA KAMA KAWAIDA
MFANYAKAZI WA TIGO MUSOMA AKIENDELEA NA MAJUKUMU
AFISA HUDUMA KWA WATEJA WA TIGO Bi Pilila Kavishe AKITOA ZAWADI KWA WATEJA WA TIGO KATIKA MAAZIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 14 BAADA YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Bi Pilila Kavishe
HAPA KAZI TU
ZAWADI KW WATEJA KAMA KAWAIDA
MFANYAKAZI WA TIGO MUSOMA AKIENDELEA NA MAJUKUMU
AFISA HUDUMA KWA WATEJA WA TIGO Bi Pilila Kavishe AKITOA ZAWADI KWA WATEJA WA TIGO KATIKA MAAZIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 14 BAADA YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Kampuni ya Tigo Mkoani Mara imesema itaendelea
kuwaunganisha Watanzania wote kupitia Mawasiliano yaliyo bora ikiwa ni kuenzi
misingi ya umoja na Mshikamano iliyoasisiwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere .
Hayo yalielezwa na Afisa
huduma kwa Wateja wa Tigo Bi Pilila Kavishe katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya
Miaka 14 ya kifo cha Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alisema kuwa kampuni ya
Tigo itaendelea kushirikiana na wateja wake katika shughuli mbalimbali za
Kijamii ikiwa ni njia ya kutambua na kuthamini Mchango wa wateja wake kwa
Kampuni hiyo.
Meneja huyo alidai
hakuna kitu ambacho kinaweza kuwaunganisha watu kwa haraka kama mawasiliano
hivyo kampuni hiyo itaendelea kumuenzi mwalimu Nyrere kwa kufanikisha
mawasiliano ya uhakika.
Alisema kampuni ya tigo
inaheshimu misingi ya Mwalimu Nyerere na katika kuienzi ni kuhakikisha Wananchi
walio wengi wanafikiwa kwa mawasiliano na kuwaweka pamoja.
Kwa upande wao wateja wa
tigo walioshirikiana na kampuni hiyo na kupokea zawadi mbalimbali kutoka tigo
walisema kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhaakikisha huduma bora
inapatikana kwa wateja ikiwemo mawasiliano ya uhakika na kuwataka kuto kurudi
nyuma.
Mmoja wa wateja wa tigo
alijitambulisha kwa jina la ingali Daudi alisema wameishukuru kampuni ya tigo
kwa kufanya kumbukumbu ya muasisi wa Taifa kwa kuboresha mawasiliano mkoani
mara na nchini kote kwa kuwa ndio uzalendo halisi.
No comments:
Post a Comment