Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars wakishangilia ushindi |
Mwakilishi na kiongozi wa Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi wa kikosi cha timu ya wasichana mara baada ya kuibuka washindi katika michuano ya kimataifa ya Airtel Rising stars |
Ni Tanzania |
Timu ya wasichana ya Tanzania imeibuka mabigwa katika michuano ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya kimataifa ya Airtel Rising Stars
yaliyokuwa yanafanyika mwaka huu nchi Nigeria.
Tanzania ilipata ubigwa huo
baada ya kuchuana vikali na timu ya Kenya katika mechi ya Fainali na
kuifunga Kenya goli moja bila na kuibuka mabingwa . Donisia Daniel ndio
alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania.
Tanzania ilikua kundi moja na
Sierra-Leone , Malawi , na Uganda. Walishinda mechi moja dhidi ya
Sierra-Leone 2-1 , wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na kutoka sare na
Malawi 1-1.
Wakashinda 4-2 katika mikwaju
ya penati dhidi ya DRC katika robo fainali mechi zilizopigwa katika
uwanja wa NIS Sports. Na wakawatoa Uganda kwa mvua ya magoli 8-1.
Mbali na ushindi huo wa
wasichana watanzania walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo , Mchezaji
bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora wa mashindano kwa
upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa upande wa wasichana
Shelda Boniface.
Kwa upande wa wavulana Timu
ya Niger wametetea tena ubingwa baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya
penati 7-6 katika mechi ya fainali ya Airtel Rising Stars ilifanyika
kweny uwanja wa Agege nchini Nigeria.
Niger wamefanya vizuri
kuanzia hatua ya makundi baada ya kushinda michezo yote katika makundi
na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu katika mechi sita .
Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda.
Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo
Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika
nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy
Pitch, National Institute for Sports Fiels na Main bowl.
Kulianza na “ gala night”
jumapili usiku ikafatia sherehe za ufunguzi , na mechi za ufunguzi za
makudi katika uwanja wa AgegeTownship .
Mashindano ya kiamataifa ya
umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya
pili , mashindano haya yamekua bora kwa vijana wadogo na kwakuzingatia
jinsia.
No comments:
Post a Comment