na Lucy Ngowi -Tanzania Daima
UCHUMI
wa Tanzania kwa kiasi kikubwa unategemea utalii wa wanyamapori, hivyo juhudi
zinahitajika kukomesha ujangili.
Mkurugenzi
wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songolwa, alisema hayo katika maadhimisho
ya Siku ya Tembo kitaifa alipokuwa akimwakilisha Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu.
Alisema
juhudi za haraka zinahitajika kuhakikisha ujangili unakoma.
“Nchi
yetu kwa kiasi kikubwa uchumi wake unategemea utalii, madini yakichimbwa
wanaondoka nayo tunabaki na mashimo, tembo wakitunzwa vizuri wakazaliana
wanabaki. Uchumi wetu umebebwa na wanyamapori, juhudi za makusudi
zinahitajika kuokoa wanyama hao,” alisema.
Alisema
ujangili unaoendelea hivi sasa nchini unasababishwa na wachache wenye uroho,
hivyo Watanzania waikatae hali hii kwa kuipinga vikali.
Kwa
mujibu wa Songolwa, kuna nchi zilizokuwa na tembo barani Afrika lakini hivi
sasa hawana, hivyo Tanzania ikicheza muda si mrefu watatoweka.
Alizitaja
nchi hizo kuwa ni Gambia, Swaziland, Burundi na Mauritania. Tanzania ni nchi
ya pili kwa kuwa na tembo wengi, inayoongoza ni Botswana.
|
No comments:
Post a Comment