MZOGA WA FARU DUME AITWAYE LIMPOPO(11)ALIYEUAWA AGOSTI 1 MWAKA HUU NA
TEMBO DUME ALIYEVUNJA UZIO WALIMOHIFADHIWA KATIKA ENEO LA NYABIKWABE
KIJIJI CHA MAKUNDUSI KATA YA NATTA WILAYANI SERENGETI,FARU HUYO NI KATI
YA WAWILI WALIOLETWA MWAKA 2007 NA KAMPUNI YA SINGITA GRUMETI RESERVES
TOKA AFRIKA KUSINI.
KUUAWA KWA FARU HUYO KUMETHIBITISHWA NA MKURUGENZI WA WANYAMA PORI
TANZANIA PROFESA ALEXANDRE SONGORWA NA KUDAI KUWA WALIKUWA KWENYE ENEO
MAALUM KAMA MRADI WA KAMPUNI HIYO,NA KUWA TEMBO DUME ALIPOINGIA KATIKA
HIMAYA YA FARU HAO KULIPELEKEA FARU KUCHACHAMAA NA KUMFUKUZA NDIPO
AKAMCHOMA KWA JINO LAKE SEHEMU YA MOYO NA KUMBANA SEHEMU YA NUNDU NA
KUFA PAPO HAPO.
MBALI NA UJANGILI WA WANYAMA HAO PIA TEMBO NA FARU NI WANYAMA WASIOPATANA NA HUISHI KWA KUKWEPANA.
No comments:
Post a Comment