Sunday, May 12, 2013

Sir Alex Ferguson na Paul Scholes ,waagwa na ushindi wa 2-1 dhidi Swansea City ndani ya Uwanja wa Old Trafford.

Sir Alex Ferguson na Paul Scholes ,waagwa na ushindi wa 2-1 dhidi  Swansea City ndani ya  Uwanja wa Old Trafford.















Meneja  Sir Alex Ferguson leo(May 12,2013)  amewasili kwenye Uwanja wa Old Trafford kuiongoza timu yake kwa mara ya mwisho.
Sir Alex Ferguson
Kocha huyo alitangaza kustaafu kuifundisha timu hiyo Manchester United  aliyodumu nayo kwa takribani miaka 27 baada ya kutwaa taji la 13 la Ligi Kuu ya Uingereza.
Mashetani hao Wekundu ambao sasa watakuwa chini ya kocha wa Everton, David Moyes kuanzia msimu ujao wamenyana na Swansea City na kushinda bao 2-1.
Aidha pia kiungo wa timu hiyo Paul Scholes nae ameamua kumfuata kocha wake kwa kutundika daluga kuitumikia klabu yake pekee katika soka la kulipwa.
Gwiji huyo wa Manchester United mwanzoni alistaafu wakati wa mwisho mwa msimu wa 2010/2011, lakini akaamua kubadili maamuzi na kurejea kwenye timu mwezi January mwaka jana.
Paul Scholes
Katika taarifa yake Scholes, 38, alisema:Hatimaye ninatundika daluga zangu kabisa!
"Kucheza soka ndio ilikuwa kila kitu kwangu, na kuwa na na mafanikio kwa muda mrefu kwenye soka ndani ya Manchester United, chini ya meneja bora kabisa wa muda wote, ni heshima kubwa. 
“Timu ipo kwenye hali nzuri na itaendelea kufanikiwa chini ya uongozi wa David Moyes.”
Scholes amecheza zaidi ya mechi 700 akiwa na jezi ya United na kesho atakusanya medali yake ya 11 ya kombe la premier league watakapocheza dhidi ya Swansea.

No comments:

Post a Comment