MTOTO WA MIAKA 4 DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI KWA HUDUMA AYA KWANZA.
WANANCHI WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA WILAYA WAKIWA NA SHAUKU YA KUMUONA MTUHUMIWA.
KINA MAMA WALIOGUSWA NA TUKIO WAKIWA NJE YA HOSPITALI KUMUONA MTOTO HUYO.
AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI
HAPA AFANDE AKIWA HOI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI..
MADAKTARI WAKIJITAHIDI KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.
MADAKTARI WAKIWA KAZINI KUHAKIKISHA WANAOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.
AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI HUKU AKIWA AMEFUNGWA PINGU.
JITIHADA ZA KUOKOA MAISHA YA MTOTO ZIKIENDELEA
INASIKITISHA SANA JAMANI
MAJUKUMU YA KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO YAKISONGA KWA KASI.
AFANDE BWIRE AKIWA NA PINGU ZAKE WODINI
MUNGU AMPE AHUENI MTOTO HUYU.
KAHAMA
Mkazi wa kitongoji cha Sango
kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), ameshikiliwa
na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa
sababu za wivu wa kimapenzi.
Tukio hilo limetokea leo
jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness (28)
Elias huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha
kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.
Kwa mujibu wa majirani, kelele
zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire akichoma
nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo
huku akiwa amefunga mlango.
Imefafanuliwa kuwa, baada ya
kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada
kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa
amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani.
Majirani kwa hasira walianza
kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya
kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia
kwenye gari kwenda kituoni.
Hata hivyo Wakati gari la
Poisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka
kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo kilichomsababishia majeraha
makubwa sehemu za usoni.
Mtoto Devotha na baba yake
Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku
Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.
No comments:
Post a Comment