Friday, May 24, 2013

Muungano wa AU washerehekea miaka 50


AU imetimiza miaka 50 tangu muungano huo kuzinduliwa 
 
Wageni mashuhuri na marais wa Afrika wameanza kuwasili mjini Addis Ababa Ethiopia kwa sherehe za kuadhimisha miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa Muungano wa Afrika.

Muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama OAU,uligeuza jina na kujulikana kama AU mnamo mwaka.

Hapo kesho Jumamosi kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka hamsini ya AU na Zitahudhuriwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na marais wengine wa Afrika.

Kauli mbiu ya sherehe za hapo kesho ni mjadala mkuu kuhusu ushirikiano wa nchi za Afrika na kuimarishwa kwa muungano huo.

Mwenyekiti wa tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili na ambacho kinaweza kufikiwa katika miaka hamsini ijayo.

Sherehe za AU zinakuja wakati swali kuu kwa AU ni kesi zinazowakabili washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007/08 Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto pamoja na mtangazaji wa redio Joshua Arap inaendelea katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

Duru zinasema kuwa huenda mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za Afrika wamekubaliana kuhusu azimio linalotaka kesi ya washukiwa hao kurejeshwa Kenya ambako inaweza kusikilizwa na hatua kuchukuliwa dhidi ya watakaopatwa na makosa.

Shereha hizi pia zinakuja wakati bara la Afrika linashuhudia migogoro nchini Mali, DRCongo huku Misri ikiwa bado haijatengamaa baada ya kufanyika mapinduzi ya kiraia yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak.

Lakini mwenyekiti wa AU ana matumaini kuwa Afrika iko kwenye mkondo mzuri wa kimaendeleo.
Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 21 wa AU, Dlamini Zuma alisema kuwa Afrika imekuwa kiuchumi katika muongo mmoja uliopita, imeshuhudia maendeleo ya kiuchumi , ustawi wa kikanda , uimarishwaji wa miundo mbinu na ushirikiano wa kikanda.

Sherehe hizi ambazo zitafuatwa na mkutano wa siku mbili wa marais wa AU, zitatoa fursa kwa wananchi wa bara la Afrika kuangazia ufanisi wa Muungano huo.

No comments:

Post a Comment